Dinsdag, Mei 22, 2018

ZIJUE SIKU HATARI ZA KUPATA MIMBA

Image result for mzunguko wa hedhi

N akama hujaelewa nipigie simu kwa 0753121916 ili nikueleweshe.

Muhimu kwanza ni kujua mke wako (au mwanamke wako sijui mkuu) ana mzunguko wa siku ngapi.
Wapo wa siku 28, 35 etc. Kufahamu hasa hesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwezi huu hadi siku ya kwanza ya hedhi ya mwezi ujao. Wengine hesabu zao ziko irregular, hapo ni mtihani kidogo.
 Wengine ni regular, yani mathalan, siku 28 kwa kila mwezi. Tutapigia mfano kuwa mtu wako ana mzunguko wa siku 28, siku ya kwanza ya mzunguko ikiwa ni siku ya kwanza kupata hedhi (na SI siku ya kwanza ya mwezi kwenye kalenda. Yani sio tarehe 1 Januari, au 1 Februari, ingawa labda ya mtu wako ikawa inaingiliana na tarehe za kalenda, hilo sifahamu).

 Sasa basi, kufahamu lini ni siku za hatari kwa mtu wako (siku za Ovulation...yani yai kutoka), chukua idadi za siku katika mzunguko wake, ambazo hapa tutaassume kuwa siku 28, toa siku 14 kutoka hapo (28-14=14). Jibu letu ni 14, hivyo siku ya 14 tangu aanze kupata hedhi ndiyo siku atakayo ovulate (yani kutoa yai). Ukikutana naye faragha katika siku hiyo kuna uwezekano mkubwa akabeba mimba.

 Aidha, wakati mwingine huwa mzunguko hauko sawa, hivyo kitaalamu unaongeza siku 2 mbele na unatoa siku 2 mbele, na kwa hivyo ukikutana naye siku ya 12, 13, 14, 15, 16 zote ni siku za hatari. Literature nyingine zinataka uongeze siku 3 mbele na siku 3 nyuma (iwe tarehe 11, 12, 13, 14, 15, 16, na 17). Na sababu nyingine kubwa ya kuongeza siku 2 (au 3) mbele na nyuma ni kuwa sperm (seli ya uzazi ya kiume) inao uwezo wa kukaa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa siku 3 (masaa 72) ikiwa hai na ovum (seli ya uzazi ya mwanamke) inao uwezo wa kukaa hadi siku 2 (masaa 48) kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke ikiwa hai. Hivyo basi, unaweza kukutana faragha na mtu wako leo, mathalani ni siku ya 12 ya mzunguko wa mwanamke wako, sperms zako zikakaa siku 2 hadi 3 zikiwa hai, zikaja kuchavusha (kufertilize) ovum yake baada ya siku 2 na ukabaki unashangaa kwanini amepata ujauzito. 

Na kama kuongezea tu, mwanamke anapofikia kwenye siku ya kuovulate (kutoa yai) huwa ana mabadiliko fulani ya kifiziolojia yanayompata. Mfano, atakuwa na joto la mwili lililopanda kiasi, atakuwa ana hamu kubwa zaidi ya kukutana faragha na mwanaume n.k, kutokana na mabadiliko ya kihomoni anayoyapata mwilini mwake wakati huo. Natumai nimejibu swali lako ipasavyo mkuu.

mubashara blog +255753121916

27 opmerkings:

  1. je mwanamke anaweza kupata mimba kwenye siku zake za hedh????

    AntwoordVee uit
    Antwoorde
    1. Hierdie opmerking is deur 'n blogadministrateur verwyder.

      Vee uit
  2. KWA KIFUPI HUWEZI PATA MIMBA SIKU ZA HEDHI NA KWA NYONGEZA TUNASHAURI SIKU UKIWA HEDHI SI VYEMA KUKUTANA KIMWILI NA MWENZI WAKO

    AntwoordVee uit
  3. Jibu la hakika ni Ndiyo! Ingawaje wanawake wengi hawawezi kushika mimba wakati wana hedhi, Kuna baina ya wengine wanaoweza kushika mimba wakati wanashirikiana ngono wkati wana hedhi. Hii si kawaida kwa wengi lakini kulingana na dakitari Jeannnette Lager, M.D, MPH aliyesomea maumbile ya wanawake, anatuelea jinsi mwanamke anaweza kushika mimba wakati ana hedhi sana sana kwa wale walio na mzunguko fupi zaidi yaishirini na nane au zaidi.

    AntwoordVee uit
    Antwoorde
    1. Hii ni mpya ya kupata ujauzito akiwa hedhini..

      Vee uit
  4. Nauliza mwanamke mfano ameona sku zake tareh 14 siku za hatar zinaanzia tarehe ngapi kama ameingia tareh hyo ya 14?

    AntwoordVee uit
  5. Nauliza mwanamke mfano ameona sku zake tareh 14 siku za hatar zinaanzia tarehe ngapi kama ameingia tareh hyo ya 14?

    AntwoordVee uit
  6. Naomba ufafanuzi docter, mimi mke wangu anamzunguko wa siku 28 yaani mwezi jana wa kuki aliingia tarehe 19 na alitegemea mwezi ujao huu wa kumi na moja ataingia tena tarehe 16, 17 au 18 je docter kwa hesabu zake yupo sawa na leo ni tarehe 27 amepitiliza je anaweza yakuwa mimba imetunga? Naomba majibu tafadhali no; 0767282461

    AntwoordVee uit
  7. Nataka kujua ukianza period tarehe 9 siku za hatari ni tarehe ngapi.

    AntwoordVee uit
  8. Mmmmmh mm nmesex sku za hatari nifanyaje kuzuia mimba

    AntwoordVee uit
  9. Swali lanngu n hivi.-- ukifanya tendo la ndoa na bado kama siku 2 aingiee bleed..jeee mimba itaingiaa???

    AntwoordVee uit
  10. Swali lanngu n hivi.-- ukifanya tendo la ndoa na bado kama siku 2 aingiee bleed..jeee mimba itaingiaa??? Kulingana na iyoo kalenda yako kuwaa siku za mwisho kuingia bleed mimba haingiii

    AntwoordVee uit
  11. Mi mpenz wangu siku zake zinabadilika badilika kila mwezi mpka sjuagi sku yake ya hatari n IPI. Naomba msaada katika hili 0718827593

    AntwoordVee uit
  12. Naomba kuuliza Mimi huwa naingia bleed tarehe 8 siku zangu za hatari ni tarehe ngapi hapo

    AntwoordVee uit
    Antwoorde
    1. kuanzia tarh 14 ndo cku za hatar mpka tareh 20

      Vee uit
  13. Je? mwanamke anaweza kupata mimba akiwa bado ananyonyexha

    AntwoordVee uit
  14. Mimi tarehe tarehe za kuingia period zinabadirika kila mwez mfano mwez wa kwanza tarehe 3 unaofuata tarehe 27 nitahesabu vipi kuzijua siku za hatari za kushika ujauzito.

    AntwoordVee uit
  15. Naomba kuuliza ikiwa umehesabu kuanzia siku ya kwanza ya kuingia period had siku ya 11 ambayo ndo siku ya kwanza ya hatari ukashiriki tendo la ndoa je hapo Kuna uwezekano wa kupata mimba?

    AntwoordVee uit
  16. doctor mke wangu yeye ana mzunguko wa 28 day's tarehe 1 mpaka 5 kamaliza.
    but this time kaingia tarehe 13 period sasa hapa kanichanganya kujuwa siku zake hatari.. naomba nisaidie nijuwe

    AntwoordVee uit
  17. Doctor nataka kujua siku zangu za hatari naanza kubleed tarehe 6 hadi 11

    AntwoordVee uit
  18. Doctor nataka kufahamu mke wangu ameanza kubleed 23,na anamaliza siku 3 mbele,je siku za hatari Ni zipi !!?

    AntwoordVee uit
  19. Kama kimfano me naanz hedh tareh 25 cku za hatar zinaanzia ngap naenda sikubtatu adi nne

    AntwoordVee uit