Vrydag, Mei 04, 2018

ZIWA NYASA LASHANGAZA ULIMWENGU KWA SAMAKI WENYE RANGI.






MBEYA- MATEMA

NA CHRISPIN KALINGA

Wakazi wa Kijiji cha Matema Wilayani   Kyela Mkoani Mbeya wamezungumza na waandishi wa habari juu ya uwepo wa Ziwa Nyasa na  wananufaika vipi kwa uwepo wa ziwa hilo na huku wengine wakisema kuwa licha ya mafanikio hapakosi changamoto.Moja ya mvuvi wa ziwa hilo anaye fahamika kwa jina la Kyando amewaambia waandishi wa habari kuwa ziwa hilo linafaida kubwa sana kwa vijana wa maeneo hayo kwa kuwapatia fedha zakujikimu kila siku kwa uvuvi wa samaki ziwani humo.

Akaongeza kwa kusema kuwa ziwa hilo limekuwa na faida kubwa kwao na hata kwa Mkoa huo na nchi kwa ujumla kwa kujipatia watalii kutoka maeneo ya nchi za jilani na baadhi ya wakinamama wa maeneo hayo wamesema kuwa ziwa hilo kwa upande wao limekuwa na faida kubwa kwa kufanya  biashara ndogondogo haswa migahawa na wakaongeza kwa kusema kuwa mwambao mwa ziwa hilo wanatengeza vyungu kwenye maeneo hayo kwaajili ya biashara.

Sambamba na hayo wavuvi wakamaliza kwakuimba serikaka kuwasaidia vifaa vya uvuvi na huku wengine wakiomba wadhamini wanaoweza kujitokeza kuwapa mitaji baadhi ya vijana ili wanunu nyavu za kuvulia samama kwa viwango stahiki.Hali kadhalika ziwa nyasa matema limezungukwa na wafanya biashara ambao huuza vinywaji na wengine kutengeneza baadhi ya maeneo hayo kwa kuyaweka vizuri kwaajili ya watalii wanao watembelea.

Msemaji  wa ziwa hilo   Bwana kyando akasema kuwa anapenda kuwakalibisha watu kutoka maeneo mbambali kwa kuja kutalii na kujione vitu vingi ndani ya ziwa hilo haswa samaki aina mbalimbali zenye rangi .
 Pia  Elasto  Cassian kiongozi wa ziwa hilo aliye fumba kitengo chake  ameongeza kwa kusema kuwa licha ya samaki hao kuna jiwe ndani  ya eneo la ziwa linalo  julikana kwa jina la PALIKYALA ‘Pana Mungu’ na akaongeza kwa kusema kuwa kuna eneo ambalo limejitenga alimaaalufu kama pango ambalo linaulefu kutoka kwenye ziwa hilo hadi makete mkoani njombe na akaweka wazi kuwa pango hilo zamani lilikuwa linatumika kwaajili ya dua mbalimbali ikiwepo kuomba mvua na kadhalika.     


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking