Maandag, Mei 14, 2018

Tanzania yaanza maandalizi ya kuridhia mkataba wa silaha za Baolojia na sumu

Serikali imesema ipo haja ya kuridhia mkataba wa kupambana na silaha za baolojia na sumu ili kuweza kutoa fursa kwa wataalamu mbalimbali nchini katika kuwajengea uwezo wa kukabiliana na athari za mashambulizi ya silaha za sumu na kibaoloji.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 11, 2018 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 28 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Jasson Rweikiza aliyetaka kujua ni kwa nini Tanzania haijajiunga na mkataba wa kupambana na silaha za sumu (Biological Weapons Convention).

"Tanzania ilisaini mkataba wa kupambana na silaha za baolojia na sumu tarehe 1 Agosti, 1972 lakini mpaka sasa haijaridhia mkataba huo, kutoridhiwa kwa mkataba huo kulitokana na kutoonekana athari zake za moja kwa moja kwa wakati huo ambapo matumizi salama ya mkataba ikiwemo utafiti wa magonjwa ya binadamu, wanyama na mimea yameendelea kufanyika nje ya mkataba huo. Changamoto zinazotokana na matishio mbalimbali ikiwemo ugaidi, zimesababisha hitaji la kuridhiwa kwa mkataba huo na kutekelezwa kwa vitendo baada ya kutungiwa sheria", amesema Dkt. Mwinyi.

Pamoja na hayo, Dkt. Mwinyi ameendelea kwa kusema

"Serikali inafahamu madhara yaliyopo hivi sasa ya kutoridhiwa kwa mkataba huo ikiwemo Tanzania kuwa katika kundi dogo la nchi ambazo hazijaridhia mkataba huo kama vile Haiti, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Misri, Somalia na Syria ambapo Tanzania kuwepo katika kundi hilo hakutoi taswira nzuri kwa jamii ya Kimataifa kwani kati ya nchi hizo nyingi zina migogoro ya muda mrefu ya ndani....

"Kuwanyima fursa wataalamu wetu kupata mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika kujenga uwezo wa kukabiliana na athari za mashambulizi ya silaha za sumu na kibaolojia na pia kunanyima fursa kwa wataalamu na viongozi wa kitanzania kushiriki kwenye uongozi wa taasisi mbalimbali za kimataifa zinazosimamia sheria za silaha za kibaolojia na sumu".

Kwa upande mwingine, Dkt. Mwinyi amesema teyari waraka umeshaandaliwa na muda si mwingi utapelekwa Bungeni kwa ajili ya kuridhiwa ambapo ameahidi mpaka kufikia Septemba 2018 utakuwa umeshawasilishwa.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking