Maandag, Mei 14, 2018

Yanga imebakiza nafasi moja kufuta machungu


Michuano ya Kombe la Kagame iliyopangwa kupigwa mwezi ujao Jijini Dar es Salaam huenda ikawa zali kwa Yanga ambayo kama ikicheza karata zake vizuri inaweza kufuta machungu ya msimu mzima wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Zawadi za michuano hiyo ya wiki tatu ni kubwa kuliko zile za Ligi Kuu  ambayo inachezwa msimu mzima nyumbani na ugenini, ingawa kwa kutwaa ubingwa wa Kagame hawashiriki popote zaidi ya kutajirika.

Bingwa wa Kagame anabeba kitita cha shilingi milioni 68 wakati bingwa wa Ligi Kuu Bara ambaye ni Simba anapewa Shilingi milioni 84.

Zawadi hizo zinawaniwa na klabu mbalimbali za ukanda wa CECAFA ambapo Tanzania itawakilishwa na Yanga, Simba na Azam FC ambao ni mabingwa watetezi endapo Yanga na Simba mmoja wao akibeba kombe hilo, anapewa bonasi ya Shilingi milioni 250 na mdhamini wao SportPesa fedha ambayo tayari ipo kwenye maandishi.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking