Sondag, Mei 06, 2018

Visa vya uhalifu wa kingono vyapitukia India

India rape arrest

Polisi upande wa Mashariki mwa India katika jimbo la Jharkhand wamearifu kuwa wamemkamata mtuhumiwa mkuu anayehusishwa na unyanyasaji wa kingono na mauaji ya binti mdogo .

Dhanu Bhuiyan na washirika wake wanashutumiwa kumchoma kwa moto msichana mwenye umri wa miaka kumi na sita akiwa hai siku ya Ijumaa.
Wazee wa kijiji wamekwisha tamka faini waitakayo kwa mtuhumiwa huyo na washirika wake baada ya ndugu wa binti kulalamika juu ya shambulio hilo la kudhuru mwili.
Polisi waliarifu kuwa adhabu waliyotoza iliwachukiza wanaume, ambao waliwapiga wazazi wa msichana kabla ya kuiwasha nyumba yao kwa moto na msichana huyo mdogo akiwemo ndani.

India rape arrest
Tukio hilo limesababisha hasira kubwa nchini kote, Watu kumi na tano wamekamatwa hadi sasa kuhusiana na ubakaji na mauaji .
Mashuhuda wa tukio awanaarifu kuwa binti huyo alitekwa akiwa nyumbani kwao wakati wazazi wake walipo kuwa wamekwenda kwenye sherehe za harusi .Baadaye taarifa ziliarifu kuwa alibakwa na wanaume wawili katika eneo la misitu karibu na kijiji cha Raja Kendua.
Baada ya kugundua shambulio hilo, wazazi wa binti huyo walikwenda kwa wazee wa kijiji kupeleka mashtaka dhidi ya wahalifu .Watuhumiwa hao na muathirika wa tukio hilo inasemekana wanafahamiana fika , kauli hii ilitolewa na mkaguzi mkuu wa polisi Shambu Thakur wakati alipokuwa akizungumza na shirika la habari la AFP.
Wazee wa baraza la kijiji hicho hawakuchukulia uzito wowote juu ya suala hilo.Hata hivyo , wazee hao wana ushawishi mkubwa katika maeneo mengi ya India ya vijijini na hiyo ni njia ya kukabiliana na migogoro bila ya kupitia mfumo wa mahakama wa India wenye gharama kubwa.
Hata hivyo, wazee kadhaa wa kijiji wamehukumiwa kwa kupitisha maamuzi kinyume cha sheria na kuwa kinyume na ushahidi ulivyo.
Tukio hilo la hivi karibuni linakuja kama Uhindi, linakuja kutoka kwenye kamba ya uhalifu wa kijinsia. Inaarifiwa kuwa kesi elfu arobaini za ubakaji ziliripotiwa nchini India kwa mwaka 2016 pekee.
Hata hivyo, matukio mengi yanaaminika kuwa yanasemwa kwa sababu ya unyanyapaa unaohusishwa na unyanyasaji wa kijinsia.
mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking