Sondag, Mei 13, 2018

Tanzania yatinga nusu fainali Kombe la Dunia


Timu ya wasichana walio kwenye mazingira magumu ya Tanzania, imetinga hatua ya nusu fainali ya fainali za Kombe la Dunia kwa watoto waishio kwenye mazingira magumu nchini Urusi baada ya kuifunga Marekani kwa mabao 5-0.

Mchezo huo wa Robo fainali ya kwanza umechezea asubuhi ya leo huko Moscow Urusi na vijana hao kutoka kwenye kituo cha TSC cha Mwanza kutoa dozi hiyo nene kwa vijana wa Marekani.

Tanzania sasa imekwenda katika nusu fainali ikiwa na imecheza mechi tatu bila kupoteza wala kuruhusu wavu wake kuguswa baada ya kushinda mechi zake mbili za hatua ya makundi dhidi ya wenyeji Urusi pamoja na Kazakhstan.

Tanzania sasa itacheza na timu ya wasichana ya Uingereza kwenye mchezo wa nusu fainali baada ya Uingereza kuifunga Bolivia mabao 2-0.  Mchezo huo utapigwa kesho saa 3:30 asubuhi kwa saa za Tanzania.

Ikumbukwe kwamba Tanzania ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo walilichukua mwaka 2014 nchini Brazil kwa kuifunga Burundi kwenye fainali iliyopigwa Rio de Janeiro.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking