Woensdag, Mei 02, 2018

WANACHUO NJOMBE WAIVAMIA MATEMA..



Picha na Francis Malekela  Baadhi ya wanafunzi walio fanya Ziara ziwa Nyasa.

MBEYA .

NA MWANDISHI WETU

Wanachuo wa Chuo cha Uandishi wa Habari Eckros School of Journalism kilicho Mkoani Njombe  wamefanya Ziara ya kimasomo katika Kijiji cha Matema Wilayani Kyela Mkoani Mbeya  kwenye Ziwa Nyasa kwa lengo la kujifunza kwa vitendo.


Wanafunzi hao wamezungumza na wakazi wanao zungukwa na ziwa hilo kwa kujifunza vitu  vingi haswa historia ya ziwa hilo kuanza kwake na hadi mahali lilipo sasa.

Moja ya mwanachuo wa Chuo hicho anaye soma fani ya Uandishi wa Habari Daniel Lameck Tumbo amesema kuwa Ziara hiyo ya Matema amejifunza mambo mengi haswa kuanzishwa kwa Ziwa hilo kuwa lilijulikana tangu zamani zilizo kadiliwa.

Aidha kijana huyo akaongeza kwa kusema kuwa ziwa nyasa lilitoka na  bonde la ufa na akaongeza  kusema kuwa ziwa hilo lina samaki aina mbalimbali lakini pia samaki wenye rangi mbalimbali waliopo kwenye ziwa hilo.


Wanafunzi hao wameongozana na Mkuu waChuo hicho pamoja na walimu wa Chuo hicho huku mkuu wa chuo hicho  Erick Mlelwa akizungumza na chombo chetu cha habari  cha Mubashara blog kwa kusema kuwa lengo la kuwapeleka wanachuo hao kufanya ziaraMkoani humo ni kuwafundisha kwa vitendo kwa lengo la kujibia mtihani yao ya mwisho .


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking