Donderdag, Januarie 11, 2018

 


WAFUGAJI LUDEWA,WALIA NA WEZI WA NG'OMBE WACHINJAJI WATAJWA,


11 January 2018

 
 

Wimbi la wizi wa Mifugo aina ya Ng'ombe limeendelea kuwatesa Wafugaji wa mifugo hiyo katika kata za Ibumi, Mundindi na Ludende wilayani Ludewa Katika Mkoa wa Njombe Baada ya Wafugaji wengi wa vijiji vya Ibumi na Amani Kudai kuwa watu wasiojulikana wamewaibia mifugo yao iliyokuwa mazizini wengine malishoni katika maeneo ya machungio. 

Wakizungumza na Mwanahabari wetu Bw. Maiko Christopher Luoga aliyeko wilayani Ludewa wafugaji hao walimweleza mwandishi kuwa Watu hao wasiofahamika Wamekuwa wakifungua Mazizi ya wafugaji kisha kuondoka na Ng'ombe wanaoamua kuwachagua wao na kutokomea nao kusikojulikana hasa katika Maeneo ya Ludewa mjini na wengine wakivusha katika mto Ruhuhu kuelekea Ng'ambo ya pili katika Mkoa Wa Ruvuma kwaajili ya Biashara haramu ya wizi. 

Aidha licha ya malalamiko hayo wafugaji pia walikuwa wakiwatuhumu mojakwamoja Wafanyabiashara wa nyama ya Ng'ombe katika maeneo ya Ludewa mjini kuwa ndio wahusika na wizi wa mifugo yao hali iliyo mlazimu mwandishi wetu kuwatafuta baadhi ya Wachinjaji wa Ng'ombe Ludewa mjini akiwemo bw. Likotiko ambae ni mfanyabiashara Mkubwa anaetuhumiwa zaidi na wafugaji na hapa Mfanyabiashara huyo anazungumza zaidi. 

Katika Hatua nyingine Jeshi la polisi Ludewa mjini Limethibitisha kuikamata baadhi ya mifugo ambayo ni ya wizi iliyokutwa katika mazingira ya kutelekezwa na wezi huku wamiliki wa mifugo hiyo wamepatikana kutoka katika kijiji cha Amani wakidai kuwa hadi sasa zaidi ya Ng'ombe 31 Wameibwa katika kijiji hicho na wengine saba kutoka katika Kijiji cha Ibumi na wanne katika Kijiji cha Ludende kuanzia mwezi December 2017 na Idadi bado inazidi kuongezeka. 

Kwaupande wake Afisa Mifugo Wilaya ya Ludewa Katika Mkoa wa Njombe Bw. Marko Mhagama Maarufu kwa jina la Mdimi Amethibitisha kutokea kwa matukio hayo ya Wizi wa mifugo katika wilaya ya Ludewa na Kusema kuwa Ofisi yake ya mifugo tayari imeshaanza kuchukua Hatua za Kutokomeza kabisa Janga hilo linalowatia Umaskini wananchi Katika Wilaya ya Ludewa kama anavyofafanua Zaidi.
Hatahivyo Afisa Mifugo wilaya ya Ludewa Bw, Marko Mhagama amewataka wafugaji wilayani humo kuendelea kuweka alama mifugo yao ili kuweza kuitambua mifugo yao pindi inapoibwa kwakuwa itajulikana popote itakapokamatwa nchini kupitia Alama zitakazoitambulisha Mifugo hiyo.

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking