Maandag, Januarie 29, 2018

MTU MMOJA AKUTWA AMEKUFA KWA KUJINYONGA WILAYANI LUDEWA MKOANI NJOMBE


 LUDEWA

 CHARS IGNATIO

Mkazi mmoja wa kijiji cha Maholong`wa kata ya Ludende wilayani Ludewa mkoani Njombe aliyejulikana kwa jina la MELANIA FRANCE LUOGA amekutwa amejinyonga juu ya mti katika eneo la maholongw`wa huku sababu za kujinyonga hazijulikani mpaka sasa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Maholong`wa Bw,BARNABA JACOBO MGIMBA amesema alipata taarifa tangu alhamisi ya kupotea kwa marehemu huyo na ilipofika January 28 mwaka huu mida ya saa tisa mwenyekiti huyo alipewa taarifa na wanandugu kuwa mtu aliyepotea ameonekana akiwa maerehemu.

Kwa upande wake msemaji wa familia ya akina France Luoga amesema marehemu huyo aliondoka tangu January 23 mwaka huu na kuelekea kusikojulikana wakati ndugu zake wakifikiria kuwa ameelekea kwa mumewe Songea ikiwa ni kawaida yake kufanya safari hizo pasipo kuwaaga ndugu zake.




chrispiny kalinga

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking