Woensdag, Januarie 31, 2018

LUDEWA MKUU WA WILAYA YA LUDEWA MKOANI NJOMBE ATOA KAULI NZITO JUU YA YEYOTE ATAKAYE KUTWA AMESIMAMA NA WANAFUNZI.





 Na chrispiny kalinga.

wananchi wilayani ludewa mkoani njombe katika kata ya mlingali na wanaulalamikia uongozi wa shule za sekondari zilizopo katika kata hizo kwa madai ya kutozwa chakula cha watoto wao kisicho pungua debe kumi ambazo ni sawa na kilo mia moja.

Hali kadhalika wananchi hao leo katika mkutano wa hadhara ambao umeongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Mh.Andrea Tsere wameziku kuongea mambomengi ambayo yanawatatiza katika uongozi wa shule mbalimbali zilizopo ndani ya kata hiyo na kusema kuwa sambamba na hilo watotot wao wanafukuzwa shule kwa madai wakale madawati kutoka kwa wazazi.

 Aidha Mkuu wa Wilaya hiyo ndipo alipo simama na kuchukua maamuzi ya kufuta michango yote iliyo kuwa ikiendelea katika shule hizo na kusema kuwa tangu siku ya leo haruhusiwa mwalimu yeyote kumfukuza mwanafunzi kwa mchango wowote ule wala kumfukuza mwanafunzi kwa kumdai dawati.

Akaongeza kwa kusema kuwa mwalimu yeyote asihusike kwenye kamati ya bodi ya chakula kama wazazi wataliziana mara mia wao wawe wanashirikishwa tu na si vinginevyo na amesema kuwa wingi wa mahindi hayo upunguzwe kwa sababu kama kila mtoto atatoa kiasi hicho maghara ya kuwekea chakuila hicho hayata kuwepo.

pia mkuu wa wilaya hiyo ametoa uamuzi mgumu kwa kusema kuwa mwalimu yeyeote atakaye mfukuza mwanafunzi katika wilaya hiyo nayeye anafukuzwa aende akaendelee na maisha yake  na amewaagiza wazazi kuwasimamia watoto wao kwa kupata elimu bora.

sambamba na hilo mkuu huyo amewataka wananchi kuto kuwa karibu na wanafunzi kwa madai haitaji mamba mashuleni na akatoa angalizo kwa kusema kuwa yeyote atakaye simama na mwanafunzi sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
chrispiny kalinga

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking