Dinsdag, April 10, 2018

KUWASA yashtumiwa kupandisha bili na kutosikiliza kero za wateja

Baadhi ya wananchi wameilalamikia Mamlaka ya Maji Safi na Taka katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma (KUWASA) kwa kuwatoza bei kubwa tofauti na matumizi halisi.

Akiongea moja kati ya waathirika na huduma hiyo Rose Mongo Mkazi wa Mji Mwema, alisema Mamlaka hiyo imekuwa haifuatilii huduma kama ipo sawa wao wanajari maslahi binafsi wanashindwa hata kutatua malalamiko ya watumiaji.
"Tumekosa imani na mamlaka hiyo kutokana na kutuletea bili kubwa wakati mwinigine maji hayatoki wao wanaleta bili kwa kukadiria,"  alisema Mongo.

Naye Diana Augustine Mkazi wa Mtaa wa Rusimbi, alieleza kuwa toka wapewe huduma ya maji mtaani hapo hawakuwekewa mita za maji na ndio lalamiko lao kubwa lakini mamlaka imelifumbia macho na pia kutokana na kuwa na vyanzo vingi vya maji katika mkoa huyo lakini maji yanatoka kwa awamu.

Kwa upande waka Meneja wa Mamlaka wa Vipimo Mkoa wa Kigoma Zainabu Kafungo alithibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo na kudai kuwa  zoezi  la kukagua na kuhakiki mita  litaendana na utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuweza kujua kusoma mita na gharama wanazolipia.

Aidha alifafanua kuwa  kwa mujibu wa Sheria ya Zabuni hawaruhusiwi  kupeleka mita kwa Mamlaka ya Maji pasipo kuhakikiwa na na Wakala wa Vipimo na endapo ikibainika umekeuka utaratibu huo sheria kali zitachkuliwa bila kujali we ni nani.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking