Dinsdag, April 10, 2018

Baada ya ligi kusimama hatimaye yarejea

Ligi Kuu ya soka la Wanawake Tanzania hatua ya Nane bora inatarajia kuendelea Jumapili Aprili 21 kwenye viwanja tofauti baada ya kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars.

Hatua hiyo ya nane bora ambayo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) iliyokuwa kambini kujiandaa na mchezo wake wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake itaendelea katika mzunguko wa 5.

Hatua ya nane bora inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ikishirikisha timu za Panama FC ya Iringa inayotumia Uwanja wa Samora, Evergreen Queens ya Dar es Salaam inayotumia Uwanja wa Karume na JKT Queens ya Dar es Salaam wanaotumia Uwanja wa Mbweni.
Timu zingine ni Alliance ya Mwanza wanaotumia Uwanja wa Nyamagana, Mabingwa watetezi Mlandizi Queens ya Pwani wanaotumia Uwanja wa Mabatini, Baobab ya Dodoma wanaotumia Uwanja wa Jamhuri.
Kigoma Sisters wanaotumia Uwanja wa Lake Tanganyika na Simba Queens wanaotumia Uwanja wa Karume. Huu ni msimu wa pili wa Ligi ya Wanawake kuchezwa ambapo katika msimu wake wa kwanza timu ya Mlandizi Queens ndio waliibuka mabingwa.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking