Saterdag, April 07, 2018

Mchungaji aanguka na kufariki madhabahuni

Image result for mchungaji
picha ya mtandaoni
Waumini wa kanisa la Katoliki katika Dayosisi ya Jimbo la Bungoma nchini Kenya, wako kwenye maombolezo baada ya mchungaji wao kuanguka na kufa papo hapo akiwa madhabahuni.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo la BungomaNorman Kong’oo Wambua, marehemu alianguka majira ya saa 8 mchana katika kanisa la Mabanga ma dakika chache mbele akatangazwa kuwa ameshafariki.
Inaelezwa kuwa kiongozi huyo alikuwa na maradhi ya figo ambayo wanahisi ndio yaliyosababisha kifo chake cha ghafla. Mwili umekwisha hifadhiwa mortuary ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking