Saterdag, April 07, 2018

Yanga yaitwanga 2-0, Dicha ya Ethiopia


Yanga imeitwanga Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kuwania kucheza Kombe la Makundi.

WaliOyokuwa mwiba mkali kwenye ngome ya Waethiopia ni Raphael Daudi aliyefunga bao sekunde 30 tu tangu mpira kuwa na Emmanuel Martin aliepachika dakika ya 54 ya kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo wa nyumbani unaifanya klabu ya Yanga kuwa na matumaini ya kusonga mbele endapo watafanikiwa kulazimisha sare au kushinda mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Ethiopia

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking