Saterdag, April 14, 2018

VIJANA WA CHADEMA WAAMIA CCM KWA KUKOSA MATUNZO CHADEMA






NJOMBE

 Na Chrispin kalinga

Wanachuo wilayani njombe katika mkoa wa njombe wameamua kuamia ndani ya chama cha mapinduzi  mkoani kutoka katika chama cha chadema.


Wakiwa na waandishi wa habari leo hii wanavyuo wa vyuo viwili Eckros school of journalism na mpechi vtc wamesema kuwa hawajaona manufaa tangu waingie katika chama walicho toka.

Hali kadhalika wanachuo hao wakaongeza kwa kusema kuwa ndani ya UVCCM wanaamini watajifunza vitu vingi na wanamuunga mkono rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzani mweshimiwa John pombe magufuli kwa utendaji wake wa kazi.

Hali kadhalika mwenyekiti wa tawi hilo ajulikanaye kwa jina la chrispin kalinga amesema ujio wa vijana hao katika umoja wa vijana wa ccm kutafanya kuimalisha chamacha mapinduzi na kufanya baadhi ya mambo kwenda kwa haraka.

Akaongeza kwa kusema kuwa amewapokea vijana kutoka chadema wasio pungua thelathini na sita nab ado wengine wanaongezeka kuingia ndani ya chama cha mapinduzi .

Pia kiongozi huyo akamaliza kwa kusema kuwa hivi kalibuni wanatarajia kuwa na mkutano wa kuwaunganisha wanachama hao na viongozi wa juu kwa kuwatambulisha rasmi na kuwakabidhi kadi za chama cha mapinduzi.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking