Saterdag, April 07, 2018

Marekani yaua wapiganaji watatu wa Al Shabab

Uongozi wa jeshi la Marekani umesema wapiganaji watatu wa Al Shabab wameuawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani ijumaa.

Katika taarifa yake jeshi la Marekani limesema, mashambulizi hayo yalitekelezwa kwa ushirikiano na majeshi ya Somalia karibu na mji wa Jilib, karibu kilomita 370 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Washington imeongeza shughuli zake za kijeshi nchini somalia, wakati ambapo Al Shabab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda, linajaribu kupindua serikali inayoungwa mkono na nchi za Magharibi na kuiweka chini ya sheria za Kiislamu.

Kundi la A Shabab lilitimuliwa katika mji wa Mogadishu mnamo mwaka 2011 na kupoteza udhibiti wa vituo vingi vya miji ya Somalia, lakini bado lipo katika sehemu nyingine za nchi na lina uwezo wa kufanya mashambulizi mabaya.

Al Shabab mara kwa mara inaendesha mashambulizi yake dhidi ya jeshi na raia.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking