Dinsdag, April 17, 2018

MIKOCHENI KUMEHARIBIKA

 MVUA zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam zimeendelea kuleta madhara katika maeneo ya Mikocheni barabara ya Chato mtaa wa Lukuledi  baada ya barabara hiyo kukatika na kujaa maji.


Akizungumza na Michuzi Blog, Kaimu Meneja uhusiano wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO) Everlasting  Lyaro ameeleza  maji hayo ni ya mvua na karavati  linalomwaga maji hayo ni yale yanayokusanywa maeneo  ya Mwenge, Mwananyamala na Mikocheni.


Aidha ameeleza walienda eneo la tukio  na kugundua tatizo hilo halikuwa lao bali ni watu  wa ujenzi wa barabara chini ya Manispaa na tayari suala hilo limekabidhiwa kwa makandarasi waliojenga barabara hiyo.


Pia ametoa rai kwa wananchi kwa kuwataka kuhifadhi miundombinu hasa mita zitakazosombwa na maji na watakaokumbwa na tatizo hilo watarekebishiwa mita hizo bure. Amewataka wananchi kutoa taarifa  kwa maeneo yatakayokosa huduma ili  washughulikie mara moja.


Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Abdul Rashid ameeleza  tukio hilo lilianza jana saa nane mchana baada ya magari kadhaa kupita ghafla barabara ilishuka na maji kuanza kumwagika hali iliyosababisha barabara kushindwa kupitika na ugumu wa biashara.
Hadi waandishi wetu  wanaondoka eneo la tukio sehemu ya barabara hiyo iliendelea kukatika.



mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking