Maandag, Desember 10, 2018

IJUE HISTORIA FUPI YA LIVINGSTONE RANGERS F.C TOKA MKOANI NJOMBE



Livingstone Rangers Football Club nitimu ya mpirawamiguu yenye makao yake katika kijiji cha Luana, wilaya ya Ludewa iliyoanzishwa Januari 2018.

Ikachukua Ubingwa wa Wilaya msimu wa mwezi wa sita hadi wa kumi na kwasasa ipo Njombe kushiriki Ligi yaMkoa Hatimaye imefanikiwa kushiriki ligi hiyo na kujipatia ushindi na umaarufu mkubwa kwa wakati mwafaka Mungu kaisadia timu hiyo ya Livingstone kuingia katika mashindano ya Ligi ya Azam Sports Federation. 

licha ya mafanikio makubwa yaliyo tokana na kuwepo kwa timu hii tangu kuanzishwa kwake kumekuwa na mambo ya msingi ambayo waanzilishi wa timu hii walilenga mambo yafuatayo-


  1. kuendeleza kudumisha mchezo wa mpira wa miguu.
  2. kuibua na kuinua vipaji vya vijana na kuufanya mpira kuwa Ajira kwao.
  3. kutoa burudani ya mchezo kwa jamii na mambo mengi yanayo endelea kufanyika kwa jamii na yanaonekana moja kwa moja.
Hivyo tangu kuanzishwa kwa timu hii Januari Mwaka 2018 imeendelea kufanya vizuri kwa kushinda Mechi za Wilaya akafuzu kuingia Bingwa Wilaya na hatimaye imeendelea kufanya vizuri katika Ligi Mkoa na imefanikiwa kwa kiasi kukubwa hadi sasa katika ligi Mkoa.
Sambamba na hayo Ligi wilaya ilipata matokeo kama ifuatavyo Tarehe 16-6 2018 ilipata ushindi wa goli Moja dhidi ya Ibumi F.c na Tarehe 20-6-2018 ilipata ushindi wa Magoli matatu bila dhidi ya timu ya Vijana Mbelu F.c na Tarehe 24-6-2018 ilipata ushindi wa Goli Mbili bila dhidi ya Stand Ludewa f.c  na tarehe 1-7-2018 ilicheza mchezo mwingine na Ibumi F.c na ikato sare ya goli moja kwa kwa moja na kuibuka na ushindi mzito wa kuongoza kwa kuzifunga timu zote hizo kwa magoli matamu kabisa.
katika hatua nyingine Livingstone Rangers F.c iliingia kushiriki ligi ya mabingwa wilaya na kuanza kuvuna mavuno mazuri kama ifuatavyo; mchezo wa kwanza ulichezwa dhidi yao na Chinga F.c na ndipo Livingstone ikazindua kwa kuwapiga kipigo cha goli moja bila na mchezo wa pili ulichezwa na bodaboda mchezo huo ulikuwa ni wa sinto fahamu Livingstone iliibuka na ushindi wa kihistoria ya kufunga magoli matano bila. Ndipo timu hiyo ikaanzwa kuogopwa kwa namna ya ubora ilio kuwa nao na mchezo wa tatu ulichezwa tarehe 21-10-2018 dhidi ya Mizani F.c na livingstone ikaibuka na ushinda  Wa goli moja bila na tarehe 23:10:2018 bado timu hii iliibuka na ushindi mkubwa wa kihistoria ya magili matatu bila dhidi ya Ujuni F.c.
pia bado timu hii ya livingstone inaendelea kufanya vizuri katika mechi ya ligi mkoa na michezo yote mitatu iliyo chezwa mkoani hapo imechukua ushindi wa point tatu kwa kila mchezo na bado ikashiria mashindano ya Azam Sports Federation na kila timu iliyo kutano nayo imeendelea kuweka Historia ya kipekee katika Mkoa wa njombe. 
Mpenzi msomaji wangu naimahi umeelewa kwa kiasi kikubwa maendeleo ya timu hii tangu kuanzishwa kwake na hadi maendeleo yake tukutane tena katika muendelezo wa makala hii pindi ligi mkoa itakapo kamilika nitakusogezea yote hapa hapa.

Makala hii imeandaliwa na 
Afisa Habari wa Timu ya Livingston. 
 Chrispin kalinga.
...........................................................................


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking