Mbunge wa (CHADEMA) Tarime Vijijini, John Heche amefunguka na kusema
ameanza kupata vitisho mbalimbali kutoka kwa watu wasiojulikana
wakimtishia maisha yake baada ya kusema ukweli kuhusu kupanda kwa
gharama za vitambulisho vya Taifa.
Akiongea na www.eatv.tv Heche amedai kuwa ameanza kupata vitisho hivyo
na kudai kuwa haviwezi kumrudisha nyuma katika kuisimamia Serikali na
kuibana Serikali na kusema hawezi kubadili msimamo wake hata siku moja.
"Mtakumbuka kuwa majuzi jioni nilizungumza bungeni kuhusu kudanganywa
umma juu ya mradi wa e-passports na kupanda kwa gharama za vitambulisho
vya Taifa. Maelezo yangu bungeni yalitokana na Taarifa kutoka Kamati ya
PAC na yalijibiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Sasa ndugu zangu
nimeanza kupata vitisho dhidi ya ‘credibility’ yangu na maisha yangu.
Ndugu zangu Taifa letu linapitia wakati ngumu Sana" alisema Heche
Heche aliendelea kusema kuwa
"Genge la wahalifu wa ki Uchumi na kisiasa kamwe lisitarajie nitatishika
ama kubadili msimamo. Vitisho vilivyoanza dhidi yangu baada ya kuibua
Ufisadi Katika Vitambulisho vya Taifa na E -Pasport havitaniogopesha
kamwe. Njia zao ovu ama kunitisha ama kutaka kuchafua heshima yangu ama
kunitengenezea kesi ama kuninifanyia alichofanyiwa Mhe. Tundu Lisu
hazitanirudisha nyuma" alisisitiza Heche
Mbali na hilo Heche ameweka wazi kuwa kwa sasa anaandaa nyaraka muhimu
ili azipeleke Bungeni kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza
ubadhirifu uliofanyika katika Vitambulisho vya Taifa pamoja na E-
Passports.
Source:to muungwana blog
Chrispiny kalinga blog