Mfumuko wa bei nchini Tanzania unaripotiwa kupungua kwa asilimia 0.2 kutoka asilimia 4.1 hadi asilimia 3.9 ,Taasisi ya taifa ya Takwimu imeeleza
Pamoja na hayo gharama za bidhaa za watumiaji imepanda kwa asilimia 1.2 ikilinganishwa na rekodi ya mwezi Januari mpaka Februari mwaka 2018.
Ongezeko hili limegusa hasa bidhaa za chakula.Baadhi ya bidhaa hizo ni mchele wenye ongezeko la asilimia 3.8,mahindi 4.1 samaki kwa 2.6, mboga za majani kwa 5.3 na unga wa muhogo kwa 1.9%.
Kwa upande mwingine bidhaa zilizochangia ongezeko hili ni mafuta ya taa, mkaa, na dizeli.
''Kitu kimoja kinachoathiri mfumuko wa bei ni chakula hata kama bidhaa nyingine zitashuka gharama bado mtumiaji hatahisi nafuu hiyo kwa kuwa matumizi yao makubwa yako kwenye chakula kwanza kabla ya sehemu nyingine''.Ameeleza mchumi Dr Abel Kinyondo kutoka taasisi ya utafiti ya kupunguza umasikini, REPOA.
''mfano unapozungumzia gharama za usafirishaji kutoka mashambani kupanda, moja kwa moja mlaji wa mwisho atapata bidhaa hizo kwa gharama ya juu'' ameeleza Dokta Kinyondo.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking