Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CZI Limited, Cyprian Musiba amelitaka Jukwaa la Wahariri kujitathmini na kujitafakari kuhusiana na matamko mbalimbali wanayoyatoa.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodom, ambapo amesema kuwa ni vyema Jukwaa hilo la Wahariri likajikita katika kuwasaidia waandishi wa habari.
Amesema kuwa Jukwaa hilo lina wajibu mkubwa wa kuwasaidia waandishi wa habari kuboresha maslahi yao lakini si kutumika kisiasa na kuichafua serikali.
Aidha, Musiba ameongeza kuwa TEF imekuwa ikitoa matamko mbalimbali ambayo hayana uhusiano wowote na waandishi wa habari, hivyo ameliasa kujikita zaidi katika kuangalia namna na kutetea maslahi ya waandishi kuliko kutumika kisiasa.
“Press Club hawajui, UTPC hawajui halafu wewe unatoa tamko, uandishi wa habari sio Dar es salaam peke yake, ni Tanzania nzima, ninachowashauri TEF tuwatengenezee waandishi wa habari mazingira mazuri ya kazi,”amesema Musiba
Hata hivyo, Musiba ameongeza kuwa Jukwaa la Wahariri (TEF) hawatakiwi kulalamika kuhusu kukosa wadhamini bali wanatakiwa kujikita katika kujenga misingi imara ya waandishi wa habari na si kutumika kisiasa kama wanavyofanya kwasasa.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking