Serikali ya Uingereza imewataka wananchi wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini hapa kila mwaka.
Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi.
Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari kwamba kwa sababu maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto.
“Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa hiyo na kuongeza:
“Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya dharura unayohitaji.’’
Pia taarifa hiyo iliwataka raia hao wa Uingereza kuwa makini wawapo barabarani kwa sababu watu wanaweza kutumia mwanya huo kufanya jambo lolote nchini hapa.
Hivyo raia hao wamepewa ushauri wa kuwasiliana na ofisi za ubalozi wa Uingereza ikiwa watahitaji msaada wowote.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking