Woensdag, Januarie 31, 2018

Katavi waondokana na changamoto ya umeme


na chrispin kalinga
Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameondokana na changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa OLIO ambao utasambaza umeme katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Waziri wa nishati Dkt Medard Kareman amefanya ziara mkoani Katavi na kukagua ujenzi wa miradi ya REA na Ujenzi wa Mashine za kufua umeme mkoani humo.
“Ujenzi wa mashine mbili kubwa za kufua  mradi wa umeme kwa  asilimia miamoja,” Waziri wa Nishati Dkt Medard Karemani alisema na kuwaagiza wafanyakazi  wa Shirika la umeme nchini TANESCO kufanya kazi usiku na mchana ili kuwahudumia wananchi .

chrispiny kalinga

Rais Magufuli awataka Uhamiaji kujiamini


 

Rais John Magufuli ameitaka Idara ya Uhamiaji nchini kutambua kuwa wanalojukumu kubwa la kulinda na kutembea kifua mbele katika kutekeleza majukumu yao.
Rais Magufuli pia amewaonya watendaji wachache wanaoendekeza vitendo vya kuiharibia sifa taifa na idara na kuwataka wabadilike haraka iwezekanavyo kwani hawatabaki salama.
"Uhamiaji mjitambue mnajukumu kubwa na nyeti na mtembee kifua mbele kwani Idara yenu ni muhimu kwani yeyote anayetaka kusafiri lazima aje hapa hata mimi, CDF au Rais Shein, ila wale wachache wanaotumia vibaya dhamana hii, kama hawataki kazi wapo watanzania wengi wanatafuta kazi.." alisema rais Magufuli.
Ameyasema hayo leo, Jumatano wakati wa uzinduzi wa hati ya kusafiria ya kieletroniki, jijini Dar es Salaam, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, pamoja na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi Pamoja na Amani Karume na mabalozi wa nchi mbalimbali.
Akizungumza na umati wa wageni na wananchi mbalimbali waliokusanyika kwenye tukio hilo, Rais Magufuli amesema, kufanikiwa kwa mradi huo ni jambo la kujipongeza kwa watanzania wote kwani ni mradi uliotekelezwa kwa fedha za wananchi na kuwasihi wananchi kuendelea kulipa kodi kwa uaminifu.
“Mradi huu utahusisha awamu nne, mradi huo umegharimu dola za Marekani milioni 57.82. sawa na shilingi bilioni 127, awali ilitakiwa kuwa Dola milioni 226 sawa na Shilingi bilioni 400, walipanga kutupiga mno ila nimshukuru Balozi wa Ireland kwa kusimama kidete na kufanikiwa kupata kampuni ya Marekani iliyochukua kazi hii kwa gharama hizo" alisema Magufuli.
Amewataka watanzania watakaobahatika kupata Paspoti hizo kuzilinda na kuitunza.
Wakati huo huo, Rais Magufuli  amemtaka Kamishna wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala kutafuta eneo litakalokuwa na hadhi ya kuwa Makao Makuu ya Uhamiaji na kuwaahidi kutoa bilioni 10 kama shukrani zake kwa kufanikisha kupunguza changamoto nyingi zilizokuwa zikiikabili Idara hiyo, zikiwemo za wahamiaji haramu, utoaji hovyo wa paspoti na vibali vya ukaaji pamoja na masuala mengine yaliyokuwa yakiitia doa Idara hiyo."Najua kuna watakaokasirika, kwasababu wana vibanda vyao hapo pembeni vya kiujanja janja". Alitania rais Magufuli.
Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wamekabidhiwa Hati hizo leo, na kwamba utaratibu wa kubadili paspoti hizo utaendelea taratibu hadi kukamilika kwake.
Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. MWIGULU Nchemba alisema, hati hizo zitasaidia kufuta makosa yaliyojitokeza ya kuwapa watu hati kwa nyaraka za kughushi pamoja na kudhibiti uhalifu wa kimtandao.wa kimtandao

chrispiny kalinga

PEMBEJEO, MBOLEA CHANGAMOTO, LUDEWA,




                                                                


wakazi wa kijiji cha ludewa mjini katika wilaya ya ludewa wanaulalamikia uongozi wa wilaya hiyo kwa madai ya kuletewa mbolea ya kukuzia mazao isiyo jitosheleza.

wakizungumza na mwandi wa habari juu ya uchache wa mbolea iliyo kuwa imeletwa katika kijiji hicho siku ya tarehe 28 mwezi huu ni mifuko mia moja na mbili tu ukilinganisha na wingi wa watu wa kijiji hicho.

hali kadhalika wananchi hao wameongeza kwa kusema kuwa licha ya mbolea hiyo kuuzwa kwa bei ya juu kwanzia sh.46000/=na wafanya biashara wengine huuza kwa sh.50000 lakini bado mbolea haitoshi na wakaiomba serikali kuongeza wingi wa mbolea katika wilaya hiyo. 

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya ludewa mh.Andrea Tsere amesema kuwa kwanzia siku ya kesho anawataka wafanya biashara wote kuleta mbolea ya kutosha na yeye ndiye atakaye toa kibari cha bei itakayo uzwa.

 chrispiny kalinga


Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi



Hivi falsafa juu ya matumizi ya  bajeti ambayo ipo  ndani ya uwezo wako ikoje? Hili ni swali la muhimu sana ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kujiuliza kataka maisha yake ya kila siku.

Nasema hivi kwa sababu moja kati ya tabia ya watu wengi huwa wanaishi nje ya bajeti ambayo wanakuwa wamepanga.

Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi

Ni rahisi sana kuwa na hasira, kukatishwa tamaa na hata msongo wa mawazo. Hiki ni kiu ambacho kila mtu anaweza akawa nacho kwenye maisha yake.

Hii ndio gharama ya passport za kielektroniki

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.  Mwigulu Nchemba amesema kuwa gharama mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki itakuwa Sh. 150,000.

Barnaba atoa siri kinachomuingizia mkwanja mrefu


u


STAA wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kipekee, Elias Barnaba amesema kuwa kitendo cha kuwatungia mastaa ngoma zao hasa wa kike kimemfanya kutengeneza mkwanja mrefu.

Shamsa apigwa stop kutumia Mitandao ya kijamii na mumewe


STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford anadaiwa kupigwa stop kutumia mitandao ya kijamii na mumewe, Chid Mapenzi na kwa muda sasa haonekani hasa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambako aliwaaga kabisa mashabiki zake.

Madee azungumzia bifu lake na Roma


BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Ngoma ya Sema, Hamadi Ally ‘Madee’ hatimaye amefungukia kile kinachodaiwa kuwa ni bifu zito lililopo kati yake na msanii mwenzake, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Madee alisema suala la uwepo wa bifu kati yake na Roma ni hisia tu zinazo-zushwa na mashabiki kutokana na vijembe wanavyo-tupiana na msanii huyo ambaye kimsingi ni mtani wake.

“Roma ni mtani wangu, mara nyingi huwa kuna masihara kati yangu na yeye, hata familia yake kwa ujumla, vile vijembe ambavyo huwa tunatupiana ule huwa ni utani tu hakuna uhalisia wowote, hatuna bifu kati yetu,” alisema Madee


chrispiny kalinga

Tanesco yapewa agizo



NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amelitaka Shirika la Umeme (Tanesco) mkoa wa Kilimanjaro kuweka mkandarasi wa kusimamia miradi ya umeme vijijini kila wilaya, ili ikamilike kwa wakati ifikapo Aprili, mwakani.

Jafo atoa agizo madarasa ya nyasi, udongo



SERIKALI imewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha wanaondoa madarasa ya tembe, nyasi na udongo kwenye maeneo yao.

Marufuku michango ya Elimu yazua mjadala kwa Viongozi


UAMUZI wa Rais John Magufuli kupiga marufuku michango ya elimu katika shule za msingi na sekondari, umezua mjadala katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kijiji chavamiwa na kundi kubwa la Fisi



WANANCHI wa Kata ya Inyeze wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelalamika kwa diwani wa kata hiyo kwa kuvamiwa na kundi kubwa la fisi  kijijini.