NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amelitaka Shirika la Umeme (Tanesco) mkoa wa Kilimanjaro kuweka mkandarasi wa kusimamia miradi ya umeme vijijini kila wilaya, ili ikamilike kwa wakati ifikapo Aprili, mwakani.
Mgalu aliyasema hayo jana akiwa katika ziara ya wilaya ya Rombo kujionea shughuli za utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini.
Mbali na uwekaji makandarasi kila wilaya, Mgalu pia ameitaka Tanesco kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wizarani kila baada ya miezi mitatu.
“Naagiza kila wilaya kuwekwe mkandarasi ili kuhakikisha ifikapo Aprili 2019, umeme unakamilika vijijini kote," alisema naibu waziri huyo.Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutawezesha sera ya viwanda kutekelezeka kwa vitendo na wananchi kupata maendeleo.
“Ziara yangu hapa mkoani Kilimanjaro imelenga ukaguaji hali ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ambapo hadi kufikia Aprili 2019 serikali inatarajia zaidi ya vijiji 100 kupata umeme mkoani hapa
chrispiny kalinga
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking