January 16, 2018
NA CHRISPINY KALINGA
MANENO MAZITO AYAONGEA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu: “Tutakamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Musoma”
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi
wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyoanza kujengwa mwaka 1980.
Alitoa kauli hiyo wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuwasili mkoani Mara kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.
Waziri
Mkuu amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa awamu,
ambapo wataanza na eneo la mapokezi na vyumba vya madaktari.
Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.
Waziri
Mkuu amesema tayari Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 ili ujenzi
uendelee. Ujenzi huo ulianza mwaka 1980, ulisimama mwaka 1987 kuanza
tena 2010.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amekagua uwanja wa ndege wa Musoma mkoani Mara ambao unatarajiwa kukarabatiwa na kuwekwa lami.
Amesema
kukamilika kwa ukarabati huo wa kiwanja hicho kutafungua fursa za
utalii ndani ya mkoa huo ambao umezungukwa na vivutio vingi.
Amesema
Serikali imedhamilria kukarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini
kikiwemo cha Musoma ili kuboresha huduma za usafiri wa anga.
Viwanja
vingine vinavyotarajiwa kukarabatiwa ni Iringa, Kilwa Masoko, Lake
Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na Songea.
Waziri
Mkuu amesema viwanja hivyo kwa sasa vinakarabatiwa na Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS), ambao wanajenga kwa gharama nafuu na kwa
viwango vinavyostahili.
Awali,
Meneja wa TANROADS, mkoa wa Mara Mhandisi Mlima Ngaila alisema
ukarabati huo utafanyika kwa awamu tatu ambapo ya kwanza itahusisha
upanuzi wa uwanja na ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege.
Alisema
barabara ya kuruka na kutua ndege ina urefu wa km. 1.6 na upana wa mita
33 ni ya changarawe, hivyo kusababisha baadhi ya ndege kushindwa kutua.
Pia,
Waziri Mkuu alikagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya
Musoma na kwamba ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.
“Shule
hii ilipewa sh bilioni 1.28 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu.
Nimekagua jengo la utawala, madarasa, mabweni, jiko, maabara na bwalo,
nimeridhika na kazi iliyofanyika.”
Shule
hiyo ni miongoni mwa shule 10 kongwe ambazo Serikali iliamua
kuzikarabati ili ziweze kurudi kama zamani na kuendelea kutumika.
Hata
hivyo Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Musoma kushirikiana
na uongozi wa shule hiyo katika kutatua baadhi ya changamoto
zinazoikabili.
Miongoni
mwa changamoto hizo ni malipo ya watumishi wasaidizi wakiwemo wapishi,
walinzi na madereva, ambapo aliitaka kuchukua jukumu la kuwalipa
watumishi hao badala ya kuacha jukumu hilo kwa Mkuu wa Shule.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking