Woensdag, Januarie 31, 2018

Viongozi wengine waliowahi kuapishwa na kujitangaza kuwa marais kama Odinga barani Afrika

 Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Jumanne aliapishwa kuwa 'rais wa wananchi' nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo Oktoba mwaka jana.

Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza kwa sherehe hiyo ya kuapishwa, ingawa alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa.

Waziri mkuu huyo wa zamani hayuko peke yake katika kujaribu kujitangaza marais, kukiwa bado kuna rais mwingine madarakani.

Wengine ni akina nani?
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi, Nigeria Moshod Abiola, Uganda Kiza Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais, na sasa Raila Odinga amejiunga na orodha hii.

Etienne Tshisekedi

Mwezi Novemba 2011, Tshisekedi alijitosa kwenye kinyang'anyiro dhidi ya mtoto wa Laurent Kabila, kisha aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha katika uwanja wa Wahanga, Kinshasa kutibuka. Baadaye, aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani.

Moshood Abiola

Nigeria, Moshood Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa rais kipindi ambacho Rais Sani Abacha alipokuwa madarakani.

Hii ni baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi, kutafuta msaada ili kumkabili Abacha katika utawala wake.

Alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi ilipofika mwaka 1995, Siku aliyoachiwa kutoka gerezani, alikutana na ujumbe wa Marekani na kuhuduria mkutano.

Baada ya kupewa chai akiwa mkutanoni alianguka na kuzimia na hatimaye kufariki dunia.

Jean Ping
Mwaka 2016 Gabon, kiongozi wa upinzani Jean Ping alijitangaza mwenyewe kuwa rais na kutoa wito kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali Bongo ameshinda.

Hata hivyo dunia nzima alijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo

Kizza Besigye
Nchini Uganda Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za kula kiapo kuwa Rais wa Uganda baada yake kushindwa uchaguzini mwaka 2016 na Bw Museveni.


chrispiny kalinga

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking