Waziri
Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya
Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na
kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais
hawakutambua majukumu yao.
Sumaye
amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la
Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu
nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa
wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge.
"Kazi
ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa
kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa
Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo
itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais.
"Watu
ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na
ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona hayo mambo wewe
kama umehama maana yake ulikuwa huelewi maana ya kuwa Mbunge"
alisisitiza Sumaye
Mbali
na hilo Sumaye alidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa hakijali
tena maslahi ya wananchi wake kwa kuwa kimeshika madaraka kwa muda mrefu
ndiyo maana wameweza kumrudisha Mtulia kugombea kwenye jimbo la
Kinondoni bila kujali mtu huyo amesababisha fedha za wananchi zaidi ya
bilioni moja ziteketee kwenye uchaguzi wa marudio wakati fedha hizo
zingeweza kutumika katika kufanya mambo ya maendeleo kwa wananchi.
chrispiny kalinga
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking