SIASA
Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Rombo wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Wakati Kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya kikiendelea madiwani watatu wa Chadema walifika eneo la kikao na kuomba wapewe fursa ya kujiunga na CCM,” Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole alisema.
Alieleza kwamba Kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Rombo kwa kauli moja waliwapokea wanachama hao wapya na Polepole akaelekeza uongozi wa Wilaya kuwapitisha katika program ya mafunzo ya Imani, Itikadi, Siasa, Masharti ya Mwanachama, Ahadi za Mwanachama na Sera za Maendeleo za CCM.
Pamoja na maelezo waliyoyatoa Madiwani hao wa Chadema katika kikao Cha Halmashauri Kuu ya Wilaya juu ya sababu zilizopelekea kujitoa kwao Chadema na kujiunga na CCM, wameelezea pia siri ya kudorora kwa Maendeleo Wilaya ya Rombo kuwa ni mpasuko uliopo kati ya Madiwani wanaomwunga mkono Mbunge wa Jimbo la Rombo Ndg. Joseph Selasini na madiwani wanaomwunga mkono Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Ndg. Evarist Silayo sababu ikiwa ni vita ya Ubunge mwaka 2020.
Madiwani waliojitoa Chadema na kujiunga na CCM leo ni Juliana Malamsha na Martha Ushaki wa Viti Maalum pamoja na Frank Lubega wa kata ya Kelamfuamokala.
wakati kuo huo, katika Kikao hicho, CCM kimewezesha kupatikana kwa Milioni 130 zitakazomaliza tatizo la maji Wilayani Rombo.
chrispiny kalinga
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking