11 January 2018
Wimbi la wizi wa Mifugo aina ya Ng'ombe limeendelea kuwatesa Wafugaji wa mifugo hiyo katika kata za Ibumi, Mundindi na Ludende wilayani Ludewa Katika Mkoa wa Njombe Baada ya Wafugaji wengi wa vijiji vya Ibumi na Amani Kudai kuwa watu wasiojulikana wamewaibia mifugo yao iliyokuwa mazizini wengine malishoni katika maeneo ya machungio.
Wakizungumza
na Mwanahabari wetu Bw. Maiko Christopher Luoga aliyeko wilayani Ludewa
wafugaji hao walimweleza mwandishi kuwa Watu hao wasiofahamika Wamekuwa
wakifungua Mazizi ya wafugaji kisha kuondoka na Ng'ombe
wanaoamua kuwachagua wao na kutokomea nao kusikojulikana hasa katika
Maeneo ya Ludewa mjini na wengine wakivusha katika mto Ruhuhu kuelekea
Ng'ambo ya pili katika Mkoa Wa Ruvuma kwaajili ya Biashara haramu ya
wizi.
Aidha licha ya malalamiko hayo wafugaji pia walikuwa wakiwatuhumu mojakwamoja Wafanyabiashara wa nyama ya Ng'ombe
katika maeneo ya Ludewa mjini kuwa ndio wahusika na wizi wa mifugo yao
hali iliyo mlazimu mwandishi wetu kuwatafuta baadhi ya Wachinjaji wa Ng'ombe
Ludewa mjini akiwemo bw. Likotiko ambae ni mfanyabiashara Mkubwa
anaetuhumiwa zaidi na wafugaji na hapa Mfanyabiashara huyo anazungumza
zaidi.
Katika
Hatua nyingine Jeshi la polisi Ludewa mjini Limethibitisha kuikamata
baadhi ya mifugo ambayo ni ya wizi iliyokutwa katika mazingira ya
kutelekezwa na wezi huku wamiliki wa mifugo hiyo wamepatikana kutoka
katika kijiji cha Amani wakidai kuwa hadi sasa zaidi ya Ng'ombe
31 Wameibwa katika kijiji hicho na wengine saba kutoka katika Kijiji
cha Ibumi na wanne katika Kijiji cha Ludende kuanzia mwezi December 2017
na Idadi bado inazidi kuongezeka.
Kwaupande
wake Afisa Mifugo Wilaya ya Ludewa Katika Mkoa wa Njombe Bw. Marko
Mhagama Maarufu kwa jina la Mdimi Amethibitisha kutokea kwa matukio hayo
ya Wizi wa mifugo katika wilaya ya Ludewa na Kusema kuwa Ofisi yake ya
mifugo tayari imeshaanza kuchukua Hatua za Kutokomeza kabisa Janga hilo
linalowatia Umaskini wananchi Katika Wilaya ya Ludewa kama anavyofafanua
Zaidi.
Hatahivyo Afisa
Mifugo wilaya ya Ludewa Bw, Marko Mhagama amewataka wafugaji wilayani
humo kuendelea kuweka alama mifugo yao ili kuweza kuitambua mifugo yao
pindi inapoibwa kwakuwa itajulikana popote itakapokamatwa nchini kupitia
Alama zitakazoitambulisha Mifugo hiyo.
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking