Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema nchi za bara la Afrika zimeazimia
kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta
maendeleo.
Taarifa
iliyotolewa leo Januari 30, mwaka 2018 na ofisi ya Waziri Mkuu imesema
Majaliwa ametoa kauli hiyo jana Januari 29, 2018 baada ya mkutano wa
viongozi wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa,
Ethiopia.
Amesema
nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango
cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi
Katika
mkutano huo ambao Majaliwa alimuwakilisha Rais John Magufuli, amesema
nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na
vijijini.
Amebainisha
kuwa nchi hizo zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia
ya Afrika Mashariki (EAC) na jumuiya nyingine za Afrika zimefikia
mapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme.
“Tanzania
iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme na sasa ina
mikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na
kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali,” amesema Majaliwa.
Katika
hatua nyingine, Waziri Majaliwa amesema malengo ya mkutamo huo
yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao
kilichopita.
Amesema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa inashughulikia masuala ya usalama na amani bara la Afrika.
chrispiny kalinga
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking