Jengo la Vyoo na Bafu Katika Stendi Mpya ya Magari Njombe Mjini.
Na Maiko Luoga Njombe, Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Mapema Leo January 23
,2018 Ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi
Njombe Mjini Mradi ambao unaendelea kwakusuasua na Mkandarasi hayupo
Saiti.
Baada ya kukagua Stendi hiyo ya mabasi Njombe, Mkuu huyo
wa Mkoa wa Njombe amebaini Kuwa kuta za Stendi hiyo zimejengwa Chini ya
kiwango kwakuwa kabla ya Kuanza kutumika tayari Kuta hizo
zimeshatengeneza Nyufa Licha ya Jengo hilo la stendi kutumia pesa nyingi
za Serikali hatahivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe amewaagiza Wataalamu
wa Ujenzi Kuhakikisha Sehemu zote zenye matatizo zinarekebishwa na Hatua
stahiki zakisheria Zinachukuliwa Kwa wote waliosababisha Upungufu huo
wa jengo la Stendi mpya ya mabasi Njombe Mjini.
Katika ziara hiyo
Mkuu wa Mkoa Wa Njombe pia Kwakuambatana na Uongozi wa chama cha
mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu wa chama hicho Mkoa wa
Njombe Bw. Hosea Mpagike na Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Bw.
Erasto Ngole kwapamoja wametembelea na kukagua Ujenzi wa Mradi wa Soko
Jipya la Wafanyabiashara Mjini Njombe Kisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe
alitoa maagizo Kwa Mkurugenzi wa mji wa Njombe Kuhakikisha ujenzi huo
unakamilika Kwa haraka ili wafanyabiashara waweze kuendelea na Biashara
zao.
Alipowasili Katika eneo la Soko kuu la wafanyabiashara
Njombe mjini Mkuu wa Mkoa Hakuwakuta viongozi wa kata ya Njombe mjini na
kupewa Maelezo kuwa viongozi hao wapo Katika kikao cha Kata ambapo Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Mh, Christopher Olle Sendeka Alitoa Amri kuwa
Viongozi hao waache kikao chao maramoja na kisha wahudhurie mkutano wa
Mkuu wa Mkoa wa Njombe akizungumza na wafanyabiashara Katika soko kuu la
wafanyabiashara Njombe Mjini. Endelea kutembelea www.maikoluoga.blogspot.com Kwa Habari zaidi |
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking