Bw,Godfrey Mbeyela Meneja wa PARETO Mkoa wa Njombe akifafanua Ubora Wa PARETO Mbele wa Baraza la madiwani Ludewa. |
Bei za PARETO kwa kilo Kulingana na Ubora wake |
Wananchi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wameshauriwa Kulima mazao yakibiashara Ikiwemo PARETO,KOROSHO, KAHAWA NK, yenye soko la Uhakika ndani na nje ya Tanzania ili kuweza kujikwamua Kiuchumi kutokana na Mazao mengi wanayolima Wakulima Wilayani Humo Ikiwemo mahindi Kukosa Soko Huku wakulima wakiishia Kukaa na mazao yao Ndani ya nyumba Bila kupata Faida.
Ushauri huo ulitolewa na Meneja wa Zao la PARETO Mkoa wa Njombe Bw, Godfrey Mbeyela wakati akifafanua Faida za Zao hilo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kwa Robo ya Pili ya Mwaka 2017 / 2018 kwakipindi cha Kuanzia Mwezi October hadi December 2017 Mkutano uliofanyika January 27 Mwaka huu 2018 Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Meneja huyo Wa PARETO Mkoa wa Njombe aliwaomba Madiwani wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kufikisha Ujumbe kwa wananchi katika Maeneo yao ili waweze Kulima kwa wingi Zao hilo la PARETO ambalo linaelezwa kuwa na Faida kubwa zaidi kwa Mkulima Kwakuwa PARETO Inavunwa mara kwa mara iwapo Shambani na Mkulima atauza Mazao yake kisha Kulipwa pesa yake kulingana na Mzigo Aliouza.
Akieleza Bei za Zao La PARETO Mbele ya Madiwani wa Halmashaurui ya Wilaya ya Ludewa Meneja wa Zao hilo Bw, Mbeyela Alisema kuwa kwa Msimu wa Mwaka 2017/2018 Pareto Imekuwa ikiuzwa Kuanzia Tsh, 3300 Hadi 2300 Kwa kilo Moja ya Zao hilo la Patreto huku akiwahakikishia wananchi wa Ludewa kuwa Kampuni inayojishuhgulisha na Zao hilo ndani na Nje ya Tanzania ijulikanayo kwa Jina la PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) Imejenga Kiwanda katika Eneo la Mafinga Mkoani Iringa Kwaajili ya Kununua PARETO Kwa wakulima watakao zalisha zao hilo.
Hatahivyo Kampuni ya PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) yenye Soko la PARETO ndani na Nje ya Tanzania Inatoa Miche Bure kwa wakulima wa zao hilo ambao wanahitaji Kulima zao hilo.
Katika Hatua Nyingine Meneja wa PARETO Mkoa wa Njombe Bw, Godfrey Mbeyela ameweka Bayana Taratibu na Ushauri wa Kuuza PARETO Kiwandani kuwa ni pamoja na Wakulima kuuza PARETO yao moja kwa moja Kiwandani ili kuboresha zaidi mapato yao na Kuongeza kuwa Wakulima wanashauriwa Kujiunga katika Vikundi kuanzia watano na kuendelea pamoja na Kupata kibali au kitambulisho kutoka kwa Uongozi wa Kijiji wanapotoka, juu ya nia yao ya Kuuza Pareto moja kwa Moja Kiwandani Wakiwa na Muhtasari wa Kuanzishwa kwa kikundi chao na Kibali cha Kijiji kisha watafika Kiwandani na Kupata Mkataba Tayari kwakuuza Pareto yao.
Bw, Mbeyela Aliongeza kuwa Wakulima Baada ya Kupewa Mkataba wataelekezwa namna ya Kupata Leseni Kutoka Bodi ya Pareto Tanzania inayowaruhusu kufanya Biashara ya PARETO kisha kijiji kinashauriwa Kutunza Orodha ya Vikundi vyake vyote na nakala itawasilishwa Kiwandani.
Nchini Tanzania Zao la PARETO Linaelezwa kustawi kwa wingi katika Mikoa wa Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania katika Mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa na Kiasi kidogo katika kanda ya Kaskazini Mkoa wa Arusha Pia Kampuni ya PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) Inamsaidia Mkulima Bora wa Pareto Kujua namna ya kuandaa Shamba la kuzalisha Zao hilo kuwa ni Pamoja na Mkulima Kuchagua eneo lenye Rutuba ya Kutosha, Kusafisha Shamba na Kuondoa magugu yote Shambani, Pamoja na Kulima vizuri shamba la PARETO.
Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh, Edward Haule pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ya Ludewa Bw, Ng'wilabizu Ndatwa Ludigija, Madiwani pamoja na Watumishi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Ludewa Wameipongeza kampuni hiyo ya PYRETHRUM COMPANY OF TANZANIA LIMITED (PCT) Kwakuamua kulifufua zao la PARETO Katika wilaya ya Ludewa kwakuwa wananchi waliamua kuacha kuzalisha zao hilo kutokana na Ukosefu wa soko hivyo kwasasa Viongozi hao wameuahidi Uongozi wa kampuni hiyo kuwa watawaelimisha wananchi ili waweze kuzalisha zao hilo kwa wingi zaidi.
chrispiny kalinga
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking