'Hitmaker' wa Ngarenaro, Dogo Janja amemchana msanii Edu Boy kwa aina yake ya uimbaji ya kuwa-diss wasanii wenzake katika mashairi yake na kudai kuwa anachokifanya ni utoto mtupu na kwamba hawezi kufaidika na lolote.
Mbele ya kamera za eNEWZ Dogo Janja amesema kwamba msanii anapaswa kuimba kitu ambacho hata kizazi kijacho kikipata fursa ya kuskiliza nyimbo zao kitajifunza kitu kupitia mashairi ya msanii husika.
Dogo Janja ameendelea kusema kwamba "mpaka sasa tunasikiliza nyimbo walizoimba wasanii wa zamani kama kina Mbaraka Mwinshehe kwa kuwa waliimba nyimbo zenye maadili na zenye ujumbe kwa jamii lakini pale unapoamka na kuanza kuandika mashairi ya kumchana msanii mwenzio huwezi kuwa na historia nzuri kwenye sanaa".
Msanii huyo amedai kwamba Edu Boy ni kama mdogo wake kwenye sanaa kwa kuwa amemkuta kwenye sanaa na kusema kuandika wimbo unaowachana wasanii wezake inakuwa kama umeamka na mawazo yako alafu unaamua kuyamalizia kwa wasanii wezako kwani anachoamini ni kwamba hata ukiwachana wasanii wezako huwezi kufaidika kwa lolote.
Chrispiny kalinga blog