Dinsdag, Februarie 27, 2018

Watu wawili watiwa mbaroni kwa kuhusika na mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Kinondoni

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Slaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Kiongozi wa chama cha Chadema Kata ya Hananasifu, Marehemu Daniel John.

MamboSasa: Ole Wenu Mtakao Andamana....Kitakachotokea Tusilaumiane

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema ni marufuku kwa mwanachi yoyote kushiriki kwenye maandamano kwani hawapo tayari kuona watu wakiandamana na kusababisa uvunjifu wa amani iliyopo.

Tundu Lissu Afunguka Mambo 6 Kuhusu Kifungo cha Sugu

Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu amefunguka kuhusu adhabu ya kifungo cha miezi mitano kwa Mbunge wa Mbeya Mjini na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.

Sondag, Februarie 25, 2018

Rais Magufuli Ashiriki Ibada Ya Misa Takatifu Iliyofanyika Katika Kanisa La Kigango Cha Mlimani Chato

Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akishiriki Ibada ya misa Takatifu katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.

Walichojadili Waziri Mwakyembe, Rais wa FIFA na CAF kuhusu uanachama wa Zanzibar

Na Anitha Jonas – WHUSM,Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)

Ahadi ya FIFA kwa Tanzania baada ya Rais Gianni Infantino kufika Nchini

Na Anitha Jonas –WHUSM , Dar es Salaam.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeahidi kuendeleza viwanja tisa nchini kufuatia kuongezeka kwa dau la pesa za

Hukumu ya Sugu Kusomwa Kesho February 26

Hatima ya mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayeshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli itajulikana kesho.

Kakobe akana kukwepa kodi,asema taarifa za TRA ni za Kisiasa

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Followship (FGBF), Zachary Kakobe amekanusha taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba kanisa lake linakwepa kodi.

Donderdag, Februarie 22, 2018

MWAMWA KALINGA AKIWA KWENYE MAJARIBIO YA RUNINGA

Mmiliki wa mtandao huu wa blog akifanyiwa majaribio na kurugenzi wa chuo cha uandishi wa habari kwa lengo la kuangaliwa kama alikuwa makini darasani


wa kwanza kushoto ni daniel lameck na wapili  alioye vaa shati ya njano ni Host wa kipindi ni Chrispin kalinga na aliye vaa kofia ni Mkurugenzi wa Chuo cha Uandishi wa habari mkoani njombe maeneo uya sabasaba na wamwisho kulia ni jeremia Makweta.
































Chrispiny kalinga blog

Msajili wa vyama aiandikia barua Chadema

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.

Ubalozi wa Marekani Montenegro washambuliwa

Ubalozi wa Marekani mjini  Podgorica   washambuliwa kwa bomu lilitengenezwa kienyeji  kwa mikono  nchini Montenegro.

Mwili wa Akwilina ulivyochukuliwa Muhimbili kupelekwa NIT kuagwa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa aliongoza msafara wa magari, likiwemo lililobeba mwili wa  mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuelekea katika viwanja vya chuo hicho kwa ajili ya kuagwa.

Jeneza lenye mwili wa mwanafunzi lilikuwa  katika gari maalumu la kubebea maiti.

Baada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, saa 10 jioni safari kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi itaanza. Akwilina atazikwa kesho 


Chrispiny kalinga blog

Wanafunzi Wazimia na Kupoteza Fahamu Baada ya Kumuona Akwilina ndani ya Jeneza

Vilio, simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.