Dinsdag, Februarie 27, 2018

RAIS MAGUFULI AONGEA NA DIAMOND PLATNUMZ KWENYE CLOUDS360


































Chrispiny kalinga blog

Nandy Na Aslay Walivyonogesha Usiku Wa Mapenzi Escape One


































Chrispiny kalinga blog

FULL HIGHLIGHTS: MAJIMAJI FC 1-2 YANGA SC (ASFC - 25/02/2018)


































Chrispiny kalinga blog

TENENDE AGRICULTURE COMPANY LIMITED YAJA KIVINGINE 2018

Tokeo la picha la SEMBE

TENENDE AGRICULTURE COMPANY LIMITED.

Kampuni ya uzalishaji waUnga wa Mahindi Wilayani Njombe Mkoani Njombe inapenda kuwatangazia watanzania wote kwa jumla kuwa wao ni Wazalishaji wa Unga aina ya Sembe pamoja na Mafuta ya kupikia ainaya Alizeti sambamba na hilo ni Wasambazaji na Wauzaji wa Jumla na lejeleja pamoja na kumfikishia mteja wao popote alipo ndani ya Nchi ya Tanzania  Kwa bei poa kabisa . 

WAKANDARASI WAZEMBE KUKAMATWA IRINGA,




















Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amesema hatasita kuwakataa mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura)  waliopo mkoani kwake endapo hawatatimiza wajibu wa kusimamia wakandarasi wakati wa kutengeneza barabara.

WATUMISHI NCHINI WATAKIWA KUWAHUDUMIA WANANCHI BILA UBAGUZI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawatumikie wananchi kwa uweledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya za Masasi na Nanyumbu kwa nyakati tofauti.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi aliwasisitiza watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alisema Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

“Watumishi wa umma lazima mtambue kwamba msimamo wa Serikali ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kiitikadi na kipato.”

Waziri Mkuu alisema ni vyema watumishi hao kuanza kujitathmini kwa sababu Serikali haitowavumilia watumishi watakaoshindwa kuwajibika kwa wananchi.

Pia aliwataka watendaji hao kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika kama zilivyoelekezwa.

Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 27, 2018.

Chrispiny kalinga blog

Saudi Arabia yawafuta kazi Wakuu wa majeshi

Saudi Arabia imewafuta makamanda wa vyeo vya juu jeshini akiwemo mkuu wa majeshi.

Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa makanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.

Taarifa hizo zilichapishwa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA, lakini hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa makamanda hao.

Vanessa Mdee atoa fursa kwa wasicha


Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee ametoa mchongo kwa wasichana,Muimbaji huyo wa ngoma Kisela kwa sasa ametangaza kutafuta madansa wa kike

TFF yabadili tena ratiba za Simba na Yanga

Shirikisho la soka nchini limebadili tena ratiba ya ligi kuu soka Tanzania Bara mara hii ikihusisha michezo ya timu za Simba na Yanga kusogezwa mbele na mwingine kurudisha nyuma.

Kwa upande wa mchezo wa Simba SC dhidi ya Stand United uliotakiwa kuchezwa jumapili ya Februari 4, umerudishwa nyuma kwa siku mbili hadi Ijumaa Februari 2, ukipigwa katika uwanja wa taifa Dar es salaam.

Mchezo huo umerudishwa nyuma ili kuipa nafasi klabu ya Simba kujiandaa na mchezo wake wa hatua ya kwanza kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri utakaopigwa Februari 7.

Kwa upande wa Yanga mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Februari 3 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro umepelekwa mbele na tarehe yake itatajwa hapo baadae.

Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 45 kwenye mechi 19, huku wapinzani wao Yanga wakiwa katika nafasi ya pili na alama 37 kwenye michezo 18. Yanga kesho itakuwa ugenini kucheza na Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu.

Chrispiny kalinga blog

Hawa ndio waamuzi watakaochezesha mechi ya Yanga vs Rollers


Shirikisho la mpira wa miguu Africa (CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6, 2018 kwenye uwanja wa Taifa saa 10:30 jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya

Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17, 2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.

Mwamuzi wa kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou, mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Afrika Kusini Gay Makoena.
Chrispiny kalinga blog

Mbowe na wenzake waachiwa kwa dhamana

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wachama hicho wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi tangu saa 6:50 mchana

Diamond Akabidhiwa Rasmi Leseni ya Wasafi TV na Wasafi Redio

Hatimaye Bosi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platinumz amepata leseni ya kuziweka hewani redio na televisheni za Wasafi zilizobatizwa jina la ‘Wasafi Radio na Wasafi TV’.

Freeman Mbowe na vigogo wengine wa Chadema waripoti polisi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wamekwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi.