Donderdag, Maart 01, 2018

Hope Hicks: Mshauri wa Trump na Mkurugenzi wa mawasiliano ajiuzulu

White House Communications Director Hope Hicks leaves the US Capitol after attending the House Intelligence Committee closed door meeting in Washington, February 27, 2018
Mkurugenzi wa mawasiliano na mmoja wa mashauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu ameachia ngazi yake,mamlaka imesema.
Mwanamke huyo wa miaka 29 aliyekuwa mwana mitindo na mfanyakazi wa kampuni ya Trump, amekuwa karibu naye kwa miaka mingi.
Anaripotiwa kuwaambia wafanyakzai wenzake kuwa amehisi ametimiza wajibu wake katika ikulu ya White House.
Yeye ni mtu wa nne aliyeshika nyadhifa wa mkurugenzi wa mawasiliano.
Msemaji wa White House Sarah Sanders amesema haijulikani ni lini haswa Bi Hicks ataondoka.
Amekanusha kuwa hatua hio inahusiana na ushahidi amabyo Bi Hicks aliutoa mbele ya kamati Congress wakati aliporipotiwa kukiri kusema uongo wa wazi kwa niaba ya Bw Trump.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Bi Hick alifanya kazi kama khatibu wa mawasiliano. Alichukua nafasi wa kuungoza idara ya mawasiliano ya White House Agosti iliopita, baada ya ufutaji kazi wa ghafla wa
Bw Anthony Scaramucci.
Kabla yake , Sean Spicer na Mike Dubke walishika nyadhifa hio

Chrispiny kalinga blog

Vifo na uharibifu mkubwa waripotiwa Ghouta Syria

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeambiwa kuwa vifo, uharibifu mkubwa na taabu vimeendelea kutokea eneo la Ghouta nchini Syria, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano

Lundenga Aitema Miss Tanzaniia

Mkurugenzi wa Kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania ya Lino International Agency LTD Hashim Lundenga ametangaza rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo kuanzia Februari 13 mwaka huu.

Habari Ziliizopo Katika Magazetii yya Leo Alhamisi ya Marchh 1

TCRA yazifungia nyimbo 15 za Wasanii.....Zimo Mbili za Diamond

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

Japan Yaipatia Tanzania Msaada Wa Sh. Bilioni 77.3 Kujenga New Bagamoyo Road Dar Es Salaam

Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen bilioni 3.78 sawa na Shilingi bilioni 77.3 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Rais Shein Apangua Baraza la Mawaziri

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amafanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilishia Wizara baadhi ya Mawaziri.

Woensdag, Februarie 28, 2018

UN: Mapigano yamezuia kusambaza misaada Ghouta, Syria

Umoja wa mataifa umesema mapigano yanayoendelea Mashariki mwa mji wa Ghouta nchini Syria yamezuia kusambazwa kwa misaada licha kukubaliana kuwepo kwa usitishwaji wa mapigano kwa saa tano.

Trump amtaja Parscale kama meneja wa kampeni zake za 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaja meneja wa kampeni zake za urais mwaka 2020.

Brad Parscale mtaalam wa mitandao, alifanya kazi katika kampeni

Atiwa mbaroni baada ya kutekeleza mauaji katika Facebook live

Prentis Robinson alifariki akijichukua kanda ya video ya moja kwa moja ya facebook Live

Maafisa wa polisi kaskazini mwa Carolina wanasema kuwa mtu mmoja alipigwa risasi hadi kufa alipokuwa akijichukua kanda ya video ya moja kwa moja katika mtandao wa facebook Live

Yanga yapewa muda wa kuimaliza Botswana


YANGA kwa sasa watakuwa na uhakika wa kuwamaliza wapinzani wao, Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa hapa nyumbani baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwafutia mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Shilole na mumewe wasaka mtoto

STAA wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameeleza kuwa baada ya kuingia kwenye ndoa miezi kadhaa iliyopita kwa sasa yeye na mumewe, Ashraf Uchebe wako kwenye harakati za kusaka mtoto.

Jenerali Mabeyo asema kuna Viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.