Woensdag, Maart 14, 2018

MAGAZETI YA LEO 14/3/2018


Image result for madhara ya unywaji wa pombe
ULEVI wa pombe ni mojawapo ya sababu kubwa ya maradhi na vifo vinavyoepukika. Neno ulevi linatumika pale ambapo utumiaji wa pombe unachukua umuhimu mkubwa kwenye maisha ya mtu kuliko majukumu mengine kama ya kazi na familia.

Karafuu kupata mafanikio makubwa


MSIMU wa mavuno ya karafuu wa 2017-2018 umemalizika rasmi huku ukitajwa kupata mafanikio makubwa kwa kuvunja rikodi katika kipindi cha miaka 10 ambapo jumla ya tani 8,470 zenye thamani ya Sh bilioni 118.2 zimenunuliwa kutoka kwa wakulima.
Msanii wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka sababu ya baadhi ya mstaa hasa wa kike kutodumu katika mahusiano.
Image result for Shamsa Ford
Muigizaji huyo amesema mahusiano ya watu maarufu hayadumu kutokana wanaingiza umaarufu wao katika mahusiano yao. Kupitia ukurasa wake Instagram Shamsa ameandika;
“Nimegundua mahusiano mengi ya watu maarufu hayadumu kwa sababu wengine huwa wanaleta Ustar hadi kwenye mahusiano, hata mtu wa kawaida akiwa na uhusiano na mtu maarufu ni mara chache sana kudumu,” amesema.
“Hasa kwa upande wa wanawake huwa tunaamini ustar ndo kila kitu kwa mwanaume kumbe sio, sasa sijui hatuna elimu ya ustar au vipi kwa hapa Bongo, maana ingekuwa ustar shida Beyonce na Jay Z wasingedumu mpaka leo na hawa ndo mastar wa dunia,” amesisitiza.
September 2016 Shamsa Ford alifunga ndoa na mfanyabiashara wa maduka ya nguo Rashidi Saidi a.k.a Chidi Mapenzi

mubashara blog +255753121916

Twiga Stars yaingia kambini kujiandaa na AFCON

Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imeingia kambini katika Hostel za Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT Mlalakuwa) kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake AFCON 2018 nchini Ghana
Image result for Twiga Stars
Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars).

Man United watupwa nje na Sevilla kwenye michuano ya UEFA, Mourinho atoa kauli nzito

Klabu ya Manchester United imeyaaga mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Sevilla kutoka Hispania.
Image result for man united
Sevilla wakifurahia ushindi

Rais wa Ufaransa apongeza utendaji kazi wa serikali ya Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Ufaransa nchini Mhe. Frederic Clavier ambaye aliongozana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Emmanuel Baudran.

MAGAZETI YA LEO 14/3/2018



Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.

Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama 'Black Hole', Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: "Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha."

"Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi."



  • Alizaliwa 8 Januari 1942 Oxford, England
  • Alipata nafasi chuo kikuu cha Oxford kusomea sayansi ya mambo asilinia mwaka 1959, kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamifu chuo kikuu cha Cambridge

Nigeria yatamani kufanya mazungumzo na Boko Haram

Serikali ya Nigeria imesema ina mpango wa kutumia njia ya mazungumzo badala ya kutumia nguvu za kijeshi ili kuwaokoa wasichana 110 waliotekwa katika mji wa Daptch hivi karibuni pamoja na wale waliotekwa mjini Chibok mwaka 2014.

Dinsdag, Maart 13, 2018

Kikosi cha Yanga chawasili Botswana

Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Gaborone, Botswana, na kufikia kwenye Hotel ya Crystal Palace iliyo na nyota 2.

Man City watua Abu Dhabi

 Klabu ya soka ya Manchester City imetua Abu Dhabi kwa ajili ya kuweka kambi ya mazoezi.