Donderdag, Maart 15, 2018
Uzinduzi wa Albamu ya Diamond Watikisa Kenya
Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amezindua rasmi albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’ jijini Nairobi na kufanya bonge la shoo akiwa na timu nzima ya WCB.
Mbali na WCB, wasanii wengine waliopada jukwaani na kutikisa katika shoo hiyo, ni msanii wa Marekani, Omario.
Albamu mpya ya Diamond imesheheni ngoma 20 kali zikiwemo alizowahi kuzitoa kipindi cha nyuma na nyingine mpya.
mubashara blog +255753121916
Waziri Mwijage Aweka Jiwe La Msingi La Ujenzi Wa Majengo Ya Viwanda....Mavunde Awataka Wajasiriamali Dodoma Kuchangamkia Mikopo Kutoka Sido
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh Charles Mwijage(MB) ameweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Majengo kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo katika eneo la Kizota-Manispaa ya Dodoma ambapo jumla ya viwanda vidogo 45 vinatazamiwa kuanzishwa kupitia utaratibu wa Clusters “Kongani” na pia kutoa mafunzo kwa Wajasiriamali mbalimbali.
Taarifa ya Sido kwa kamati ya Bunge yakataliwa
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imesusia kupokea taarifa ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido), huku ikitoa onyo kwa wateule wa Rais John Magufuli kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kwa kasi inayohitajika.
Agizo hilo limetolewa leo Machi 15, 2018 mkoani Singida ambapo kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Sadiq walipofika kutembelea viwanda kadhaa mkoani humo na mwenyeji wao alitakiwa kuwa ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Akizungumzia leo, Sadiq amesema kamati ya Bunge inapotembelea anapaswa kuwapo waziri, naibu waziri au katibu mkuu, lakini “tumemkuta naibu katibu mkuu na maofisa wengine wa wizara na wale wa Sido, ambao hawakuwa wamejindaa na tumeikataa taarifa yao.”
Amesema Mwijage alipaswa kuwapo wameelezwa amekwenda Morogoro kuhudhuria ufunguzi wa kiwanda cha Sigara eneo la Kingolwira.
“Kwa sasa tupo tu tunatembea tembea hapa Singida, lakini tuseme hawa watendaji wa Rais Magufuli wanapaswa kujitambua na kutekeleza wajibu wao. Kama wameshindwa kutoa ushirikiano kwetu hata kwa kumtuma naibu waziri (Stella Manyanya) au katibu mkuu, hii Tanzania ya viwanda kweli itakuja kama hakuna ushirikiano,” alihoji Sadiq.
Sadiq ambaye ni mbunge wa Mvomero amesema, “tumsaidie Rais Magufuli na sisi katika taarifa yetu tutajua kipi cha kufanya tutakaporudi Dodoma, kwa hiyo sisi kama wabunge hatujapenda kilichotokea leo.”
mubashara blog +255753121916
Serikali ya Tanzania yaidhinisha matumizi ya dawa za asili kutibu nguvu za kiume

Hivi karibuni nchini Tanzania kumeshamiri kwa uwepo wa matangazo mbalimbali ambayo mengine ni rasmi na mengine sio rasmi kuhusiana na dawa za asili haswa za kuongeza nguvu za kiume lakini sasa serikali ya nchi hiyo imethibitisha matumizi ya dawa tano za asili.
Na Maiko Luoga Ludewa
Wadau Wenye Viwango mbalimbali vya Elimu na Uchumi Ambao ni wazawa wa wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wanaoishi Nje ya Ludewa wameshauriwa Kurudi wilayani Ludewa ili kusaidia Shughuli Mbalimbali za Maendeleo zinazofanywa na Wananchi katika Vijiji na Katika kata mbalimbali wilayani Ludewa.
Teken in op:
Plasings (Atom)