Na Maiko Luoga Ludewa
Wadau Wenye Viwango mbalimbali vya Elimu na Uchumi Ambao ni wazawa wa wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wanaoishi Nje ya Ludewa wameshauriwa Kurudi wilayani Ludewa ili kusaidia Shughuli Mbalimbali za Maendeleo zinazofanywa na Wananchi katika Vijiji na Katika kata mbalimbali wilayani Ludewa.
Ushauri huo ulitolewa juzi march 13.2018 na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mh, Monica Mchilo Wakati alipokuwa Mgeni Rasmi Kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere katika Shughuli ya Uzinduzi wa Jengo la Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Madunda Iliyopo katika Kata ya Mawengi, Lililojengwa na wafadhiri kwaushawishi wa Mkurugenzi wa Shirika la PADECO Mkoa wa Njombe Bw, Wilbard Mwinuka Ambae Ni kijana Kutoka Ludewa.
Akisoma Taarifa ya Ujenzi wa Bweni hilo La wasichana Mbele ya Mgeni Rasmi na Wananchi waliojitokeza Katika Mkutano wa Ufunguzi wa Bweni hilo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Madunda Mwalimu Livino Msuku Alisema kuwa Jengo hilo Kubwa na la kisasa Limejengwa kwa Nguvu za Ufadhiri wa Profesor Ludwiq Kutoka Ujerumani kwakushirikiana na Wananchi wa Kata Ya Mawengi na Jengo hilo litakuwa na Uwezo wa Kuhifadhi Jumla ya Wanafunzi wakike 90.
Alisema Ujenzi Huo Ulianza Rasmi Mwezi September 2017 na Kukamilika Mwezi huu March mwaka 2018 Ambapo Jengo hilo limegharimu Jumla ya Tsh, 100,187,500/= Kati ya Hizo Pesa za Mfadhili ni Kiasi cha Tsh,80,150,000/= Na Nguvu ya Wananchi Ni Tsh, 20,037,500/=, Kwakutumia Pesa hiyo Jengo Limekamilika kilakitu ikiwemo Vyoo,Bafu, Umeme,Maji Pamoja na Samani mbalimbali za Ndani.
Hata hivyo Mh, Zembwela Willa ni Diwani wa Kata ya Mawengi Pamoja na Wadau mbalimbali wa Kata hiyo ya Mawengi Licha ya Kumshukuru Mfadhiri Huyo pia wamempongeza Mkurugenzi wa Shirika la PADECO Bw,Willbard Mwinuka kwa jitihada zake za Kumshawishi Mfadhiri huyo Kutoka Nchini Ujerumani na kufanikisha Ujenzi Jengo hilo la Kisasa Katika Shule ya Sekondari Madunda wilayani Ludewa.
Katika Hatua Nyingine Mkurugenzi wa Shirika la PADECO Lenye makao yake makuu Njombe Mjini Bw, Wilbard Mwinuka Kwakushirikiana na Wadau wa maendeleo Kutoka ndani na nje ya Tanzania jana Jumatano walizindua Mradi wa Maji Katika Kijiji cha Luana Kesho Alhamisi watazindua Mabweni Mawili katika Shule ya Sekondari Chief Kidulile Ludewa Mjini na Siku ya Ijumaa Wadau hao watazindua Mradi wa Maji katika Kijiji cha Maholong'wa Kata Ya Ludende wilayani Ludewa.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking