Katikati Ni Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere akiwa na Muhandisi wa maji Ludewa Nasib Mlenge wakwanza kulia na Katibu wa Vijana CCM Wilaya ya Ludewa Kushoto. |
DC Ludewa Andrea Tsere Akipanda Mti Kandokando ya Chanzo cha Maji Mapetu. |
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bi.Monica Mchilo ambae pia ni Diwani wa kata ya Ludewa Akipanda mti. |
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Ludewa Bw. Matenus Ndumbaro akipanda Mti. |
Muhandisi wa Maji Ludewa Injinia Nasibu Mlenge Akipanda mti |
Na Maiko Luoga Ludewa,
Kila Ifikapo March 22 ya Kila mwaka Tanzania Huungana Na Nchi Nyingine Kuadhimisha Siku ya Maji Duniani Ambapo kwa Mwaka huu 2018 Maadhimisho hayo yamefanyika March 22 Katika Maeneo mbalimbali hapa nchini yakiongozwa na Kaulimbiu isemayo "Hifadhi Maji na Mfumo Wa Ikolojia kwa maendeleo ya Jamii.
Wananchi wa Vijiji mbalimbali wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe kwakushirikiana na Viongozi wao wa Vijiji na Kata walianza kuadhimisha Wiki ya Maji Duniani Tangu March 16 Mwaka huu kwakufanya Usafi katika Vyanzo mbalimbali vya maji vilivyopo katika Maeneo yao.
Viongozi na Baadhi ya Wananchi Wilayani Ludewa Siku ya juzi march 22 Wamefanya Maadhimisho ya kilele cha Wiki ya maji Duniani Kiwilaya katika Kata ya Ludewa kwakupanda Miti na kufanya Usafi kwenye chanzo kikubwa cha Maji mapetu kilichopo nje kidogo na Ludewa mjini Wakiongozwa na Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Mh. Andrea Tsere Aliyekuwa Mgeni Rasmi.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha Wiki ya maji Duniani Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh. Andrea Tsere amewahimiza wZairianshi wilayani humo kutunza mazingira pamoja na kulinda vyanzo vya maji kwani kwa kufanya hivyo kutaboresha ustawi wa mazingira.
Kwaupande wake Muhandisi Wa maji Wilaya ya Ludewa Injinia Nassibu Mlenge amesema kuwa Kupitia Kilele cha Wiki ya Maji Zaidi ya Miti 200 Aina ya Midobole ambayo ni Rafiki na maji imepandwa katika Chanzo cha maji Mapetu Chanzo ambacho kitasambaza maji kwa wingi katika mitaa mbalimbali ya Ludewa mjini.
Gregory Mwinuka ni Kaimu Meneja Wa Mamlaka ya Maji Wilaya ya Ludewa amefafanua kuwa Mradi Wa Maji Mapetu Umefikia Asilimia 51 ya utekelezaji ambapo kwasasa Mamlaka inaendelea na Kazi ya Kuchimba mitaro pamoja na Kumalizia Ujenzi wa Tank kubwa la Maji Ludewa mjini Baada ya Kukamilika Mitaa mingi ya Ludewa haitakuwa na Tatizo la Maji
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking