Sheria mpya ya vyombo vya habari nchini Tanzania ambayo ilipitishwa na rais wa nchi hiyo mnamo Novemba 2016, imeanza kusikilizwa rasmi leo katika mahakama ya Afrika Mashariki huko, Arusha, Kaskazini mwa Tanzania.
Kesi hiyo ilifunguliwa mwezi Januari 2017 na wanaharakati pamoja na wataalamu katika tasnia hio ya habari, wakiwa wanaamini kwamba sheria hio inakiuka mkataba wa Afrika Mashariki kwa kuminya uhuru wa habari na uhuru wa watu kujieleza katika nchi hio.
Madai ambayo wameyaainisha na wanaona kuwa sheria hiyo imekeuka ni kwa jinsi ambavyo Waziri amepewa mamlaka ya kuvifungia vyombo vya habari na kuwepo kwa ugumu kwa wageni kupata vibali vya kuja kuandika taarifa zao nchini humo.
- Uvamizi Clouds: Wahariri Tanzania kususia habari za Makonda
- Wadau wa vyombo vya habari wakutana Tanzania
Mkataba wa Afrika mashariki unataka kila nchi lazima ikuze demokrasia na uhuru wa kujieleza.Ingawa wanaamini kuwa hakuna uhuru ambao hauna mipaka lakini sheria hii inafanya uhuru usiwepo.
Aidha baraza la habari nchini Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu wanasema sheria mpya ya habari imetoa vifungu vinavyokandamiza tasnia hiyo ya habari katika kutoa taarifa.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa rasmi kwa njia ya maandishi kwa sasa ili kiini cha mgogoro uweze kupatikana.
Wadau wa habari walidahi kuwa walitoa maoni yao wakati sheria hiyo ikiwa inaandaliwa lakini wanadhani kuwa ushauri wao haukuzingatiwa hivyo inabidi irekebishwe tena.
Mwaka jana, magazeti manne ya Tanzania Daima , Mawio, Mwanahalisi, na Raia Mwema yalifungiwa kwa muda wa kati ya siku 90 hadi miaka miwili.
- Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la Daima kwa siku 90
- Gazeti la Mawio lapigwa marufuku Tanzania
- Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la mwanahalisi kwa miaka 2
- Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la Raia Mwema kwa siku 90
Miaka ya hivi karibuni, sekta ya habari Tanzania imekua kwa kasi kubwa, lakini pia vyombo vya habari vimekuwa vikimulikwa kwa karibu sana na serikali huku sheria na kanuni zikiwa zimepatiwa mamlaka kuwazuia waandishi na mashirika ya habari kwa misingi ya usalama wa taifa na maslahi ya umma.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking