Donderdag, Maart 15, 2018

Umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo vya Silaha Sudani Kusini,wakiwemo wachochezi

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa linatarajiwa kuridhia azimio lilioandaliwa na Marekani,linalotishia kuiwekea vikwazo vya silaha Sudani Kusini,na vikwazo dhidi ya wale wanaokwamisha jitihada za kuvimaliza mojawapo ya vita vibaya barania Afrika.


Azimilo hilo linalenga kuziongezea shinikizo pande zinazohasimiana wakati zinajiandaa kwa awamu mpya ya mazungumzo ya amni nchini Ethiopia mwezi ujao kwa lengo la kuvimaliza vita vilivyodumu kwa miaka minne katika taifa hilo changa barani Afrika.

Katika hatua nyingine,Azimio hilo pia litaiongezea muda mamlaka ya tume ya kulinda amani ya Umoja wa mataifa (UNIMISS),nchini humo kwa mwaka mmoja, na kuendelea kuwekwa kikosi cha kikanda kilichopelekwa baada ya mapigano makali kuzuka Julai 2016.


mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking