Jana March 12. 2018 Wakili Alberto Msando ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa atawasilisha hoja ya kwamba Msanii Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na msokoto wa Bangi kwamba hana kesi ya kujibu.
Msando
ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kupitia Wakili Constantine Kakula kufunga ushahidi wa Jamhuri uliokuwa na mashahidi 5.
Wakili Msando amedai kuwa wanaomba kuwasilisha hoja ya kwamba mshtakiwa Wema Sepetu na wenzake hawana kesi ya kujibu.
“Tunaomba upande wa utetezi tujenge hoja ya kuwa washtakiwa hawana kesi ya kujibu na tutaiwasilisha March 23,2018 ambapo tutaeleza sababu za hoja hiyo,”-Msando.
Awali kabla ya kueleza hayo, Wakili wa serikali Kakula alimuongoza shahidi wanne Steven Alphonse ambaye ni Mjumbe wa Shina mtaa wa Nazareth Basiaya kutoa ushahidi wake.
Alphonse amedai kuwa February 4,2017 alipigiwa simu na mtu asiyemjua kwamba anahitajika na Askari Polisi nyumbani kwa Wema Sepetu.
“Nilipofika kwa Wema kuna mtu alijitambulisha kwangu kuwa yeye ni Mkuu wa Upelelezi wa Dar es Salaam na wapo eneo hilo kwa ajili ya kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema,”.
Alphonse amedai kuwa kabla ya kuanza kwa ukaguzi huo, Dada yake Wema (Nuru) aliwauliza Askari hao kama anaweza kuwakagua kabla ya wao kuanza upekuzi wao, ambapo walimkubaria.
“Dada Wema aliwapekua kwa njia ya kuwapapasa mwili baada ya hapo akawaruhusu wafanye ukaguzi wao, ambapo ulianzia Jikoni, kisha chumbani kwa Wafanyakazi, chumba cha kuhifadhia nguo na viatu vya Wema na chumba chake cha kulala” -shahidi Alphonse
Shahidi Alphonse amedai kuwa jikoni kwenye makabati ya vyombo ukapatikana msokoto 1 ambao hujatumika, pakti ya Lizra na kwenye chumba cha kuhifadhia nguo na viatu wakakuta kipisi cha Sigara.
Pia wakakagua chumba cha wafanyakazi na kukuta ganda la Kibiriti ndani yake likiwa na vipisi vya sigara.
“Pia tukaingia chumba anacholala Wema lakini Askari hawakukuta kitu chochote kabisa,” ameeleza Alphonse.
Shahidi mwingine aliyetoa ushahidi wake ni Ofisa wa Polisi D603 Detective Copro Robert. ambapo amedai February 6,2017 alipokea vielelezo vilivyokutwa nyumbani kwa Wema kisha akavihifadhi na kuvipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Copro Robert amedai kuwa katika vielelezo hivyo ambavyo ni msokoto 1 na vipisi 2 vinavyodhaniwa kuwa vya Bangi vilimuhusu mshtakiwa Wema Sepetu tu na sio washtakiwa wenzake.
Baada ya kutolewa kwa ushahidi huo, Wakili Kakula aliieleza mahakama kwamba upande wa mashtaka unafunga ushahidi wake wa mashahidi 5, ambapo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi April 3,2018.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking