Baada ya hapo anasema waliendelea kuwasiliana kwa miaka kadhaa, Bi Daniels anasema mara ya mwisho kuwasiliana ilikuwa mwaka 2010, wakati alipoahirisha kugombea useneta.
Hata hivyo tetesi kuhusu uhusiano wao zilianza kujionyesha mwezi Novemba 2016 wakati wa uchaguzi wa urais.
Jarida la Wall Street liliripoti siku kadhaa kabla ya kura kuwa bi.Daniels alikuwa kwenye mijadala kwenye kipindi cha asubuhi cha televisheni ya ABC ''Good Morning America'' kueleza yote kuhusu mahusiano yake, kabla ya kuyakata ghafla mazungumzo.
Kwa nini hii ni habari kwa sasa?
Mwezi Januari, Jarida la Wall Street lilichapa makala iliyodai kuwa Wakili wa Trump, Michael Cohen, alimlipa dola za Marekani 130,000 mwanadada huyo mwezi Oktoba mwaka 2016, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi.
Jarida linasema pesa hizo zilikuwa ni sehemu ya makubaliano ambayo hayakufahamika,ambayo alisema hakuweza kujadili masuala yake mbele ya Umma.
Ripoti nyingi zilitolewa kuhusu hayo lakini shutuma zilikanushwa vikali wakati wakielekea kwenye uchaguzi, maafisa wa Ikulu wameeleza.
Bwana Cohen alikana madai ya kumlipa pesa mwanadada huyo, katika taarifa yake kwenye jarida na kuita shutuma hizo kuwa hazina maana.Na wamekua wakipinga hilo kwa miaka kadhaa.
Lakini mwezi Februari alitangaza kuwa alimlipa Bi.Daniels pesa.
Katika taarifa aliyoitoa kwa New York Times, Bwana Cohen alisema si kampeni za Trump wala Taasisi yake iliyojua chochote kuhusu malipo,ambayo aliyatoa kutoka mfukoni mwake mwenyewe. Alisema hakurejeshewa pesa.
''Malipo kwa Bi Daniels yalikuwa yamefuata sheria'', haikuwa mchango wa kampeni wala si kwa matumizi ya kampeni.
Muda mfupi baada ya makala ya jarida hilo, Bi Daniels alizindua kampeni yake aliyoiita ''Make America Horny Again'' akisafiri kwenda South Carolina kwenye vilabu vya dansi za utupu wakati wa sherehe za maadhimisho ya kuapishwa kwa Donald Trump.
Meneja wa klabu,Jay Levy alisema alihitaji huduma yake, hiyo ilikuwa siku moja baada ya Jarida la the Wall Street kuchapisha makala kuhusu malipo ya dola za kimarekani 130,000.
Kipeperushi kuhusu sherehe hizo kilikuwa kina mzaha kusu mahusiano. Kikieleza ''alimuona moja kwa moja'' ''unaweza kumuona pia''.
Kinachoendelea sasa
Bi Daniels siku ya Jumanne alisema anamshtaki Trump, akidai kuwa hakuweka saini makubaliano yao ya kutoyaweka wazi mahusiano yao.
Mwanasheria wake, Michael Avenatti, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu mashtaka yakihusishwa na nyaraka zilizowasilishwa kwenye mahakama ya California.
Siku iliyofuata, ripoti zilisambaa zikisema Rais Trump alishinda kizuizi dhidi ya Bi Daniels.
Amri hiyo ya kizuizi ilimpa marufuku Bi Daniels kutoa taarifa za siri, kuhusu kinachoelezwa kuwa uhusiano wake na Trump.
''Kesi hii ilishafanyiwa suluhisho, kama kitafanyika chochote mbali na hicho, nitafikisha kwa mshauri wa nje wa Rais'' alieleza katibu wa habari wa Ikulu Sarah Sanders siku ya Jumatano.
Mwanasheria wa Daniels amesema kuwa kauli hiyo ya Ikulu ni ''kichekesho''.
Shirika la habari, CNN liliripoti Alhamisi kuwa Rais Trump amekasirishwa na kauli ya Sanders, kwani ni mara ya kwanza kwa mtu kutoka Ikulu kuashiria kuwa Trump alikuwa kwa namna yeyote akijihusisha na Bi Daniels.
Maoni ni yapi kuhusu hayo?
Mbunge wa Congress kutoka South Carolina, Mark Sanford ni mmoja kati ya wachache waliotoa maoni, aliliambia gazeti la Washington Post kuwa madai hayo ''yanafedhehesha mno''.
Wabunge wa Democrats Ted Lieu na Kathleen Rice, wanaowakilisha jimbo la California na New York wamelitaka shirika la upelelez FBI kuchunguza malipo yaliyofanywa na Cohen kwa Bi Daniels.
Ina maana gani kwa Trump?
Shutuma hizi zimekuja wakati mgumu kidogo kwa maafisa wa White house, na hazioneshi dalili yoyote ya kuisha.
Mbali na kuwepo kwa uchunguzi kuhusu mahusiano yake na Urusi, maafisa wa Trump wamekuwa kwenye kikaango.
Hali hii ni kama inaleta kivuli cha aliyekuwa rais wa Marekani. Kumbuka Bill Clinton alikumbwa na tishio la kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye baada ya kusema uongo kuhusu uhusiano wake na staffer Monica Lewinsky.
Lanny Davis, mwanasheria aliyekuwa mshauri wa Rais Clinton, siku ya Jumatano aliwashutumu viongozi wa Republican kwa ''kusema uongo'' kwa namna wanavyomtendea Rais Trump tofauti na walivyofanya kwa Clinton.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking