Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema ilikuwa ni lazima kwa timu yake "kurejesha uungwaji mkono wa mashabiki tena" baada ya kufikisha kikombo mkimbio wa kushindwa mara tatu Ligi ya Premia kwa ushindi wa kuridhisha dhidi ya Watford.
Licha ya takwimu rasmi kuonesha mashabiki 59,131 walijitokeza kutazama mechi hiyo, viti vingi havikuwa na mashabiki Emirates, huku ikionekana wazi kwamba baadhi ya mashabiki wenye tiketi za kutazama mechi msimu mzima walivunjwa moyo na matokeo ya klabu hiyo.
Mabao ya Shkodran Mustafi, Pierre-Emerick Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan yaliwapa vijana hao wa Wenger ushindi wao wa kwanza ligini tangu walipowalaza Everton 5-1 mnamo 3 Februari.
"Tumekuwa na kipindi cha kusikitisha na mashabiki wetu waliumia sawa na tulivyoumia," alisema Wenger baada ya mechi.
"Lakini kazi yetu ni kufanya vyema na kusalia pamoja hata mambo yanapokuwa magumu, na kuhakikisha mashabiki wanarudi kutuunga mkono."
Watford, ambao wamelazwa mara ya pili sasa katika mechi sita, walikosa bahati pale Petr Cech, ambaye alifikisha mechi yake ya 200 bila kufungwa Ligi ya Premia, alipokomboa mkwaju wa penalti kutoka kwa Troy Deeney.
Cech ndiye kipa wa kwanza kucheza mechi 200 bila kufungwa Ligi ya Premia.
Ushindi huo wa Gunners umewaacha alama 12 nyuma ya Liverpool walio nafasi ya nne, ambao wamo nafasi ya mwisho ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Arsenal hata hivyo bado wanaweza kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao iwapo watashinda Europa League, na mechi ya marudiano ya ligi hiyo dhidi ya AC Milan iliathiri uteuzi wa kikosi cha Wenger Jumapili.
Arsenal wanaongoza 2-0 dhidi ya miamba hao wa Italia na watacheza mechi ya marudiano hatua ya muondoano nyumbani Alhamisi.
Wenger alifanya mabadiliko sita kwenye kikosi chake.
Aaron Ramsey na Laurent Koscielny walipumzishwa, na Jack Wilshere akawekwa benchi.
"Nilichagua kikosi changu kuwa na nafasi ya kushinda mechi hiyo lakini pia nikapumzisha baadhi ya wachezaji ambao sikutaka waumie. Hatuko mbali sana kabla ya mwisho wa msimu, hivyo mchezaji akiumia sasa, hutaweza kumchezesha kipindi kilichosalia cha msimu."
Cech alivyosubiri muda mrefu kuweka rekodi
Cech alipookoa penalti alifikisha mechi 200 Ligi ya Premia bila kufungwa, lakini alisubiri muda mrefu sana kwani mechi yake ya 199 bila kufungwa ilikuwa 16 Desemba dhidi ya Newcastle.
"Imetuchukua mechi 18 za msimu huu kwenda mechi tisa bila kufungwa, nilifika 199 kisha nikasubiri mechi 11 kupata tena mechi bila kufungwa," alisema Cech.
"Ilikuwa inasikitisha kiasi lakini sasa tumesalia na mechi nane na lazima tuhakikishe kwamba tunashinda zote. Naamini nimefika mbali hivi kutokana na bidii yangu."
Wenger alimsifu mlindalango huyo wa miaka 35 na ksuema: "Ni ishara ya kazi kubwa ambayo Petr Cech ameifanya katika uchezaji wake, mechi 200 bila kufungwa ni ufanisi mkubwa na kwamba ameokoa penalti kufika hapo. Ni bahati kwamba ilikuwa dhidi ya Deeney.
- ‘Msitarajie Wenger ajiuzulu Arsenal’
- Wenger: Nilitafutwa na PSG nikawakataa
- Wenger ni mbinafsi amsema Sutton
"Hali yake [Cech] imeonesha jinsi mchezo wa soka ulivyo, wiki moja ametoka jehanamu na kwenda paradiso.
"Rekodi kama hiyo inahitaji kujitolea sana na ujuzi wa hali ya juu kwa sababu hauwezi kukaa muda mrefu hivyo katika mchezo huu iwapo hauna ujuzi na ustadi."
Nini kinafuata?
Arsenal watacheza nyumbani dhidi ya AC Milan Alhamisi katika Europa League, ambapo wanaongoza 2-0 kutoka kwa mechi ya kwanza. Watarejea ligini 1 Aprili dhidi ya Stoke.
Watford watakutana na Liverpool ugenini Jumamosi ijayo.
mubashara blog +255753121916
Geen opmerkings nie:
Plaas 'n opmerking