Dinsdag, Maart 20, 2018

Kushoto ni Naibu katibu mkuu wa UWT CCM Bara akizungumza jambo na DC,Ludewa Mh,Andrea Tsere Kulia
Na Maiko Luoga Ludewa

Naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM, UWT Tanzania Bara Bi, Evah Kihwele Amefanya Ziara ya Siku Mbili Tangu juzi March 18 mwaka huu wilayani ludewa katika Mkoa wa Njombe na Kuzungumza na Wanawake ambao ni Wanachama  wa UWT Wilaya ya Ludewa.


Akizungumza na wanawake wa Kata za Madope, Ludende na Ludewa Mjini Naibu Katibu mkuu huyo amesema kuwa lengo kuu la Ziara Hiyo katika wilaya ya Ludewa ni kuwashukuru wanawake wilayani Ludewa kwakufanikisha Uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika Mwishoni mwa mwaka 2017 pamoja na Kuwakumbusha wanawake kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwakani 2019.

Akiwa katika Kata ya Madope na Ludende Juzi March 18 Mwaka huu 2018 Wilayani Ludewa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi,Kihwele Alitembelea na Kukagua baadhi ya Vikundi vya Ujasiliamali vinavyoundwa na Wanawake wenye nia ya Kujikwamua kiuchumi huku Akisikiliza Changamoto zao.

Katika ziara hiyo ya Siku mbili wilayani Ludewa Naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya UWT Taifa Aliambatana na Katibu wa Idara ya Organization UWT Taifa Bi, Rizicki Kingwande, Katibu wa Hamasa na Chipukizi UV,CCM Mkoa wa Njombe Bw, Johnson Mgimba Pamoja na Bw, Lucas Nyanda Ambae ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe.

Aidha Naibu katibu mkuu wa UWT Taifa Akiwa Ludewa Mjini Ametembelea na Kukagua Kikundi cha Wanawake cha Ufugaji wa Kuku cha Tumaini Jema Chenye makao yake makuu katika Eneo la Ibani Ludewa Mjini pamoja na kikundi cha Lukolo kinachojishughulisha na Uuzaji wa Samaki katika Soko kuu la Samaki Ludewa Mjini Ambapo Changamoto Kubwa ni Uhaba wa Mitaji.

Kiongozi huyo wa Jumuiya ya Wanawake Taifa UWT Ameahidi Kuchangia Kiasi cha Tsh,100,000/= Katika kikundi cha Wanawake cha Tumaini Jema cha Ludewa Mjini ili waongezee katika Mtaji wao wa Ufugaji wa Kuku.

Katika Hatua Nyingine Viongozi hao wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe na Taifa kwa ujumla wakiongozwa na Katibu wa ccm Wilaya ya Ludewa Bw, Bakari Mfaume walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere kwa lengo la Kupata Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya ccm Ambapo wote kwapamoja wameridhishwa na Utendaji wa kazi wa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa na kumpongeza kwa juhudi zake.

mubashara blog +255753121916

Geen opmerkings nie:

Plaas 'n opmerking