Woensdag, April 04, 2018

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo

Lulu atoa mchango wake akiwa gerezani



Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye kwa sasa anaendelea kutumikia kifungo chake jela ametoa mchango wake wa Pads kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike katika kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na uongozi wa EATV.

Rais Magufuli amteua Mkemia Mkuu wa Serikali mpya


Rais John Magufuli amemteua Dk Fidelice Mafumiko  kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Rais Magufuli Kuzindua Ukuta Katika Migodi ya Tanzanite


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Ijumaa hii Aprili 06, 2018 kwenye uzinduzi wa ukuta kwenye migodi ya Mirerani mkoani Arusha.

Dinsdag, April 03, 2018

Kesi ya Mbowe na Viongozi Wengine wa CHADEMA Kusikilizwa April 16


Upande wa mashtaka wa kesi inayowakabili viongozi saba wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iruhusu kesi hiyo isikilizwe kwa haraka, ikiwezekana jambo hilo kuanza kesho.

Saterdag, Maart 24, 2018

Serikali yafunguka kuhusu kufungia mitandao

NA ISMAEL MOHAMED


Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt. John Magufuli imekanusha taarifa ya kufungia mitandao ya kijamii kama inavyoelezwa na baadhi ya watu na kuitaka jamii kuzipuuza endapo watakutana nazo mitandaoni.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa asubuhi ya leo katika ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema taarifa hizo ni uzushi mtupu hazina ukweli wowote ambayo imetengenezwa na wahalifu wa mtandao.

Jela Miaka Minne kwa Kosa la Kumpa Mimba Binti yake

Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora imemhukumu mkazi wa Manispaa ya Tabora, Sadick Masunzu (47) kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 16 na kumpatia ujauzito.

MAASKOFU WANENA MANENO MAZITO

Bwana wetu Yesu Kristo mfufuka, alipowatokea wanafunzi wake wakiwa wamejifungia ndani kwa hofu ya Wayahudi, aliwasalimu na kujifunua kwao kwa salaamu ya kuwatakia amani. 

Watu 27 wakamatwa kwa madai ya kuchoma kituo cha polisi

Watu 27 wanashikiliwa mkoani hapa kwa tuhuma za kuchoma moto kituo kidogo cha Polisi cha Mwandoya katika Wilaya ya Meatu na kuteketeza samani na mali zote zilizokuwa zikitumiwa na jeshi hilo.

Video Queen wa ngoma ‘Natamba’ Ya Aslay Akanusha Kutoka Nae Kimapenzi

Video Queen katika ngoma ya Aslay ‘Natamba’ amefunguka kuhusu taarifa za kutoka kimapenzi na muimbaji huyo.

MWANAFUNZI APIGWA NA RADI AFARIKI LUDEWA,


Na Maiko Luoga Ludewa.

Tukio lililotokea siku  March 20 mwaka huu la Kupigwa na Radi Wanafunzi 26 Katika Shule ya Msingi Itundu iliyopo katika Kata ya Mlangali wilayani Ludewa katika Mkoa Wa Njombe Limesababisha Kifo cha Mwanafunzi Mmoja Aliyeitwa Sophia Msemwa aliyekuwa na Umri Wa Miaka 12 Mwanafunzi Wa Darasa la Sita.

KILELE CHA MAJI, MITI YAPANDWA LUDEWA

Katikati Ni Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere akiwa na Muhandisi wa maji Ludewa Nasib Mlenge wakwanza kulia na Katibu wa Vijana CCM Wilaya ya Ludewa Kushoto.
DC Ludewa Andrea Tsere Akipanda Mti Kandokando ya Chanzo cha Maji Mapetu.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bi.Monica Mchilo ambae pia ni Diwani wa kata ya Ludewa Akipanda mti.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Ludewa Bw. Matenus Ndumbaro akipanda Mti.
Muhandisi wa Maji Ludewa Injinia Nasibu Mlenge Akipanda mti

Na Maiko Luoga Ludewa,

Kila Ifikapo March 22 ya Kila mwaka Tanzania Huungana Na Nchi Nyingine Kuadhimisha Siku ya Maji Duniani Ambapo kwa Mwaka huu 2018 Maadhimisho hayo yamefanyika  March 22 Katika Maeneo mbalimbali hapa nchini yakiongozwa na Kaulimbiu isemayo "Hifadhi Maji na Mfumo Wa Ikolojia kwa maendeleo ya Jamii.

ZAIDI YA WANACHAMA 320 WAJIUNGA NA UWT,CCM CHUNYA,MBEYA

Wanachama wapya wa CCM Wakila kiapo cha Uadilifu wa Chama mbele ya Mgeni Rasmi