Hali ya usalama mkoani Iringa leo imeendelea kuwa shwari licha ya tishio la maandamano yaliyotarajiwa kuwepo huku ulinzi ukiimarishwa katika baadhi ya maeneo yenye mkusanyiko mikubwa kama benki na vyuo vikuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu yeyote ataye jaribu kuuchezea muungano atashughulikiwa vikali hata kama atakuwa nje ya nchi.
Rais Magufuli katika kuadhimisha Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa 3,319 ambapo wafungwa 585 wataachiwa huru leo, na 2,734 wamepunguziwa adhabu zao.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue, Posta.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ametolea ufafanuzi suala ambalo limeanza kushika hatamu mitandaoni la kukamatwa kwa Katibu wa Baraza la Wanawake CHADEMA kata ya Kisutu Elizabeth Mambosho na kupelekwa rumande akiwa na mtoto mchanga.
Msanii Diamond Platnumz amemfagilia mrembo Vanessa Mdee kutokana na jitihada zake anazofanya kila kukicha za kuupambania muziki wake uzidi kufika mbali zaidi.
Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuigiza filamu moja na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kwani Mwenyewe hakutaka mama yake ajiingize Kwenye sanaa.