Donderdag, April 26, 2018

NAFASI ZA MASOMO HIZI HAPA .....



TANGAZO

Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Eckros school of journalism

kinakutangazia nafasi za masomo kwa

Wahanga wa mafuriko Jangwani wapata neema...tizama video live hapo chini



Familia zaidi ya 600 zilizoathiriwa na

India: Wanafunzi 14 wafariki katika ajali ya treni

Watu 14 wafariki katika ajali ya treni iliotokea baada ya kugonga basi la wanafunzi Uttar

Boti yapinduka Ziwa Victoria

Watu wawili wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakitumia kusafiria kupinduka. Ilipokumbwa na dhoruba kali katika ziwa Victoria, Sengerema jijini Mwanza.

Akizungumza na www.eatv.tv kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, amesema boti hiyo ilikuwa na jumla ya watu watano ambao walikuwa wa wakisafiri kutoka Sengerema kuja Mwanza, na ndipo ilipokumbwa na dhoruba wakiwa njiani, na kusababisha boti hiyo kupinduka na watu hao kufariki.

“Kuna boti ilikuwa inatoka Sengerema kuja huku Mwanza, ilikuwa imebeba mkaa pamoja na udaga, walivyokwenda kama robo safari yao hali ya hewa ikawa mbaya kukawa na dhoruba, wakiwa wanageuza wanarudi ikawa shida ikapinduka, ndani ya hiyo boti kulikwa na watu watano, wanaume wanne mwanamke mmoja, watatu waliweza kuogelea lakini hawa wawili walishindwa, mwanamke na mwanaume mmoja, majina bado sijayapata”, amesema Kamanda Msangi.

Kamanda Msangi amesema miili ya watu hao imepatikana, na wanafanya utaratibu wa kuihifadhi hospitali, ili ndugu waweze kuitambua na kuichukua kwenda kuzika.
Chanzo cha habari muungwana.


mubashara blog +255753121916

Mzee Kilomoni atoa nasaha zake kwa Simba kuelekea mechi dhidi ya Yanga Jumapili hii.

Mwanachama aliyesimamishwa na uongozi wa klabu ya Simba kufuatia sekeseke la kufungua kesi mahakamani kupinga mabadiliko, Mzee Hamis Kilomoni, ametoa nasaha zake kwa Simba kuelekea mechi dhidi ya Yanga Jumapili hii.

Simba yawasili Dar

SIMBA SC tayari wapo mjini Dares Salaam tangu mchana kwa maandalizi ya mwisho ya pambano dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumapili Uwanja wa Taifa.

Mzee Akilimali afunguka kuhusu Yanga

Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameomba wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuendeleza umoja ndani ya timu yao ili iweze kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Simba.

Kauli ya Balozi Dkt Slaa kuhusu Watanzania walioandamana nchini Sweden

Wakati polisi wakitoa tahadhari kwa wananchi kuhusu maandamano yaliyoratibiwa kwenye mitandao ya kijamii na kupangwa kufanyika leo, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa amesema ofisi yake ilipokea barua kutoka polisi wa nchi hiyo kuhusu taarifa za Watanzania waliotaka kuandamana jana.