Woensdag, Mei 09, 2018

Yleez Tz ASEMA AJA KIVINGINE

Image may contain: one or more people
Msanii wa mziki wa bongo fleva Yleez Tz anaye kuja kwa kasi ya ajabu katika kundi la wanamziki chipukizi amekiambia chombo chetu cha habari cha mubashara kuwa anazidi kufanya vizuri katika sakata la utunzi wa nyimbo kwaajili ya watanzania.

 Na Yleez  Tz amesema kuwa licha ya changamoto anazo kutana nazo lakini anazimudu anaamini siku moja atakuwa kama wasanii wengine wanao kimbizana katika mziki.
mubashara blog +255753121916

WAFANYA BIASHARA NJOMBE WAKIMBILIA KWA WATEJA

Image result for wafanyabiashara
Picha na Yohana Ndone

NJOMBE 

Na Nimrod Mgoye.

Serikali ya kijiji cha idundilanga katika Wilayani Njombe Mkoani Njombe  ikumbukwe kwamba miezi kadhaa iliyo pita ilitoa tamko kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la njia panda ya magereza waondoke na kuelekea katika soko mpya lililopo katika mtaa wa joshoni.

Makonda awaonya Wakandarasi Dar


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza Barabara za chini ya kiwango na kuharibika ndani ya muda mfupi jambo linalosababisha hasara kwa serikali na usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.

Tanzania yafungua ubalozi wake Israel, Mahiga aomba Israel ifungue ubalozi Dar es Salaam

Dkt Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel jijini Tel AvivHaki miliki ya pichaFOREIGN TANZANIA
Image captionDkt Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel jijini Tel Aviv
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.

Al-Shabab wampiga hadi kifo mwanamke aliyedaiwa kuolewa mara 11 Somalia

Wanamgambo wa kiislamu wanadhibiti maeneo kadhaa nchini SomaliaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanamgambo wa kiislamu wanadhibiti maeneo kadhaa nchini Somalia
Mwanamke mmoja amepigwa na mawe mpaka kifo nchini Somalia baada ya mahakama moja inayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu, al-Shabab kumkuta na hatia ya kuolewa na wanaume wengi.

Ebola: Kenya yachukua hatua baada ya watu wawili kuthibitishwa kuwa na Ebola DR Congo

Mlipuko wa mwisho wa Ebola DR Congo ulikuwa 2017 ambapo watu 4 walifarikiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMlipuko wa mwisho wa Ebola DR Congo ulikuwa 2017 ambapo watu 4 walifariki
Serikali ya Kenya imeimarisha doria katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta na vituo vingine vya mpakani baada ya visa vya ugonjwa wa Ebola kuripotiwa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shamsa Ford Amjia Juu Harmonize Kwa Kuingilia Ndoa Yake

Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.

Uingereza, Ufaransa, Ujerumani Zasikitishwa Na Maamuzi ya Trump Kujiondoa Mkataba wa Nyuklia wa Iran

Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani, ya kutangaza kwamba nchi hiyo inajiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa mpango wa kuizuia Iran kutengeneza silaha za nuklia, JCPOA, imepokelewa kwa hisia kinzani na wabunge wa Marekani na viongozi mbalimbali ulimwenguni kote.

TMA yatabiri ujio wa mvua kubwa kwa siku tano

Mvua kubwa yatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Mwanasayansi wa Australia kuuliwa na sindano ya sumu kesho

Mwanasayansi aliyesafiri kutoka Australia mpaka Uswiss David Goodall,  kwa ajili ya kuukatisha uhai wake kesho inatarajiwa kuwa ndiyo siku ya kuhitimisha maisha yake ya duniani baada ya madaktari kuchomeka sindano ya sumu katika mshipa.

TANZANIA YATIKISA ULIMWENGU KWA KUGUNDUA DAWA YA UKIMWI

Serikali imesema tayari nchi imeanza rasmi majaribio ya dawa kinga mpya inayozuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi (PrEP), huku ikikanusha kuwapo kwa dawa inayotibu ugonjwa huo.

Sondag, Mei 06, 2018

Visa vya uhalifu wa kingono vyapitukia India

India rape arrest

Polisi upande wa Mashariki mwa India katika jimbo la Jharkhand wamearifu kuwa wamemkamata mtuhumiwa mkuu anayehusishwa na unyanyasaji wa kingono na mauaji ya binti mdogo .